Bukobawadau

MITAA YA BUYEKELA BUKOBA NA CAMERA YETU

Camera yetu leo Alhamisi April 21,2016 tupo mitaa ya Buyekela ndani ya Manispaa ya Mji Bukoba
Mjini Bukoba kama hakuna kitakachofanyika juu ya wakazi wa Manispaa waliojenga kwenye mawe maeneo ya Kashura ikiwamo Buyekela kwa juu, basi tujue kipindupindu tutaisikia kwa mara nyingine,Mkuu wa Mkoa wa Kagera asimamie ujenzi wa mfumo wa maji taka kwa gharama ya wakazi wa milimani,ukweli ni kwa mbamba kwa sasa kuna baadhi ya watu wamejenga milimani sawa na walivyofanya Mwanza. Hawa waliojenga milima hiyo hawana mahala pa kuchimba mashimo ya vyoo au mashimo ya maji taka (septic tanks).
 Buyekela Bukoba barabara inayoelekea  Nyakanyasi na upande wa pili inaelekea Bandarini na upande wa kulia upo mkondo wa Mto kanoni ,Mvua zikinyesha maji yanatiririsha mpaka mto Kanoni
 Hali ya Mazingira ya mitaa ya Buyekela dhahama ni pale mvua zikinyesha na kukusanya uchafu kutoka mlimani na kutitririka mpaka Mto Kanoni unao sukuma uchafu mpaka Ziwa Victoria.
Changamoto kubwa kwa wakazi wa Buyekela ni hali ya barabara
  Masikani kwa Mdau mpambanaji Justin James
 Ujenzi wa nyumba ya Mdau Justin James (Snoop ) ukiendeleajirani na masikani yao Buyekela
Mdau Justin James (Snoop ) akiwa Site Buyekela 
 Baadhi ya wakazi wa Maeneo haya wanamiliki maeneo makubwa nyumba na mashamba yanayoruhusu hewa safi,hapa ni masikani kwa Mdau Kalokola maarufu kama 'Jojo'
Taswira katika picha kutoka mitaa ya Buyekela na Camera yetu leo Alhamisi 21,2016
Next Post Previous Post
Bukobawadau