Supastaa wa Malawi Tay Grin awapania Diamond na Vanessa
Rapper na supastaa wa Malawi, Tay Grin, amedai kuwa ana
mpango wa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. Tay ambaye hivi karibuni aliachia video ya wimbo ‘Chipapapa’aliomshirikisha msanii wa Nigeria, 2 Face Idibia, amesema kuwa hao ni wasanii
wa Tanzania anaowakubali zaidi.
“Ningependa sana kufanya kazi na wasanii wa Tanzania,”
anasema Tay.
“Napenda jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoimba. Ni
kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na
ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na
muziki wao wa Bongo Flava. Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na
wasanii hawa wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina
matumani ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo,” ameongeza.
Tay amesema anawakubali wawili hao kutokana na jinsi
wanavyojituma na mapenzi yao makubwa kwenye muziki.
“Nimekuwa nikifuatilia kazi zao kwa muda sasa na naweza
kusema kuwa wamenishika.”
Tay ni msanii anayeheshimika zaidi nchini Malawi na
amewahi kutumbuiza mara mbili kwenye shindano la Big Brother Africa na amewahi
kutajwa zaidi ya mara tano kuwania tuzo za Channel 0.
Amewahi kushirikisha wasanii kama Sway (UK), Brick &
Lace (Jamaica), Naeto C, Ice Prince, na 2face wa Nigeria), Wahu na Nameless wa Kenya,
Double HP, Da Les na Lira wa Afrika Kusini na wengine.