Watoto wa kike 20,000 kunufaika na Mfuko wa Graca Machel mkoani Mara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (kulia) akiongea na Mama
Graca Machel (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akiongea na Mama Graca Machel (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam
Mama Graca Machel akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akiongea na Mama Graca Machel (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam
Mama Graca Machel akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene
(kulia) akiagana na Mama Graca Machel (kushoto) mara baada ya mazungumzo
ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
Na Rebecca Kwandu
Watoto wa kike 20,000
kutoka mkoa wa Mara watanufaika kwa fursa ya kupata elimu kupitia Mfuko wa
Graca Machel (Graca Machel Trust) ambao umejikita katika kusaidia wanawake na
watoto nchi kadhaa za Afrika.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.
George Simbachawene mara baada ya mazungumzo na Mama Graca Machel
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
“Ni fursa nzuri ya
kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kuwasaidia watoto wetu wa kike kielimu
ambayo itawasaidia kutoka katika jamii ya umasikini na kuhakikisha wamepata
fursa ya kuvuka umri wa vishawishi na maamuzi yasiyo sahihi” alisema Waziri
Simbachawene.
Watoto hao
watakaonufaika na Mfuko huo mkoani Mara watatoka katika shule 104 ambapo
inatarajiwa kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi mara baada kuanza kutoa huduma
hiyo mkoani humo.
Waziri Simbachawene
amesema kuwa Mama Graca Machel amechagua kuja katika Tanzania kutokana
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji kwa kuzingatia mchango
mkubwa wa Tanzania kwa nchi hiyo.
Aidha, Waziri
Simbachawene amemshukuru Mama Graca Machel kwa kujali na kuuchagua mkoa wa Mara
ambao ndio mkoa alipozaliwa Mwasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa upande wake Mama Graca
Machel amemshukuru Waziri Simbachawene kwa mapokezi na ushirikiano alioupata
katika Serikali ya Awamu Tano iliyopo madarakani na kuahidi kuendelea
kusirikiana nao ambapo anaamini mpango wa kuwasaidia watoto wa kike kupita
taasisi yake utapanuka na hatimaye kuweza kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi
kupitia mikoa yote nchini.
“Lengo ni kuwabakisha
watoto wa kike shuleni ili wapate elimu, ni lazima tusaidiane wote, tuna kila
sababu ya kusaidiana” alisema Mama Graca Machel.
Uhusiano wa Tanzania na
Msumbiji ni wa kihistoria kwani wananchi wa nchi hizo walishirikiana katika shughuli
mbalimbali chini ya mwavuli wa unasaba na ushirikiano katika biashara na
tamaduni kwenye miji ya Unguja, Kilwa, Lindi na Mtwara kwa upande wa Tanzania
na katika miji ya Chilimbo, Tete, Pemba na Sofala nchini Msumbiji.