WAZIRI NAPE AHAIDI KUIHAMISHIA WIZARA YAKE KWENYE MIKOA NA HALMASHAURI ZA WILAYA KWA WADAU WA WIZARA HIYO
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye leo tarehe 14 April, 2016 akiwa mkoani Kagera ahaidi kuihamishia Wizara
yake kwenye mikoa na Halmashauri za Wilaya kwa wadau wanaohusika ili kurasmisha
shughuli na majukumu ya wizara hiyo ili iweze kupata ufanisi.
Baadhi ya wanahabari pichani
Akiongea na wadau mbalimbali wanaohusika na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuja mikoani
kujionea changamoto mbalimbali za wizara yake ili aweze kuzifanyia kazi kwa
kuishusha wizara kwa wadau wanaohusika ili kutekeleza majukumu yake.
Katika kikao hicho Waziri Nape alisema kuwa sekta nne ambazo
ni Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zimekuwa hazifanyi kazi zake vizuri
kutokana na watendaji wake kutokuwa na idara au vitengo vinavyohusika moja kwa
moja na kazi zao jambao ambalo linawafanya kujishikiza katika sehemu au idara
nyingine.
Sekta ya Habari
Mhe, Nape aliagiza Halmashauri za Wilaya kuajiri Maafisa
Habari katika Halmashauri ambazo hazina Maafisa hao, pili kuwaruhusu Maafisa
hao kuingia kwenye vikao vyote vya maamuzi ili kuweza kuzisemea taasisi hizo. Na
kutenga bajeti kwa Maafisa habari hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa
ukamilifu.
Kuhusu changamoto ya vitendea kazi Mhe. Nape alisema kuwa
Wizara yake imeanza kuwajibika kwa kuto IPad
za kisasa kwa Maafisa Habari waliopo Mikoani na katika Halmashauri za
Wilaya ili ziweze kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha, kwa mkoa wa
Kagera alitoa Ipad tano kwa Maafisa habari.
Aidha, Mhe. Nape aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa
maslahi yao yataboreshwa chini ya usimamizi wake kama Waziri mwenye dhamana ambapo alisema kuwa Serikali
ipo kwenye mchakato wa kukamilisha Mswada wa huduma kwa vyombo vya habari ambao
utazingatia mahitaji na maslahi ya waandishi wa habari.
Sekta ya Michezo
Katika sekta ya Michezo Mhe, Nape aliwakumbusha Makatibu
Tawala wa Mikoa wao kama Wenyeviti wa kamati za michezo za mikoa kutembelea na
kukaa na viongozi wa vyama vya michezo kuwakumbusha majukumu yao na kupitia
mara kwa mara mipango kazi yao ya kazi
aidha, kusimamia upatikanaji wa viongozi wenye wajibu katika michezo na
siyo vibarua wa kuingia kuwatumikia baadhi ya watu Fulani.
Aidha, alimuagiza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba na
Wenyeviti wa Halmashauri kuhakikisha
wanasimamia urudishwaji wa viwanja vilivyoporwa na kutopitisha ramani za
mipango miji zisizozingatia utengwaji wa maeneo ya wazi ya michhezo.
Sanaa
Mhe. Nape alisema kuwa
Serikali inakusudia kuirasmisha sanaa kuwa shughuli za uchumi badala ya kuwa
shughuli za burudani tu kwasababu kwasasa sanaa inaonekana kuwa ni kuburudisha
tu wakati imekuwa ikitoa ajira kwa vijana wengi. Aidha, Serikali inakusudia
kuwasimamia wasanii kuondokana na matapeli wanaonufaika kupitia kazi zao nao
kubaki hoi hae.
Katika Sekta ya Utamaduni
Mhe, Nape alisema Serikali inakusudia kutumia utamaduni kama nyenzo ya utalii
katika taifa la Tanzania
Ili kutatua changamoto zinazoikabili Wizara ya Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo zilizopo katika mikoa na Halmashauri za Wilaya Mhe. Nape alisema Wizara yake
imeanza kufanya mazungumzo na Ofisi ya Rais TAMISEMi ili kuanzisha vitengo au
idara katika Mikoa na Halmashauri za Wilaya.
Baada ya kuongera na
wadau Mhe. Nape alitembelea Uwanja wa Kaitaba na kujionea maendeleo ya
ukarabati wa uwanja huo ambapo amewahakikishia wadau wa michezo wa Mkoa wa
Kagera kuwa atahakikisha anamsukuma mkandarasi ili akamilishe uwanja huo mapema
iwezekanavyo.
Sehemu ya wadau wa maendeleo na michezo Baadhi ya wanahabari pichani
Sehemu ya wadau waliohudhuria mkutano huo wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye leo tarehe 14 April, 2016