IJUE NUSU YA MWEZI WA SHAABANI
IJUE NUSU YA MWEZI WA SHAABANI
UTANGULIZI:
Ikiwa leo ni tarehe 20 Mei 2016 ni sawa na tarehe 13 mwezi Shaabani 1437H. Wakati naandika makala hiiniko katika Miji Mitakatifu ya Makkah na Madinah katikakutekeleza ibada ya Umra ili kupata fadhila za mwezihuu wa Shaabani. Pamoja na hayo niko hapa pia katikamaandalizi ya ibada ya Hija ambapo sisi wasimamizi nawaratibu wa ibada HIJA tunatakiwa tuwe tumekamilishataratibu zote za Mahujaji watarajiwa kabla au wakati wamwezi mtukufu wa Ramadhani. Maandalizi haya nipamoja na kuandaa nyumba za kulala Makkah naMadinah, usafiri wa ndani ya Saudia, chakula namambo mengine.
Nikiwa hapa niliuliza ili kujua waumini wa miji hiimitakatifu wanachukuliaje juu ya mwezi huu waShaabani. Baadhi ya waislamu nilioongea naowanaonyesha kufurahishwa sana na ibadazinazofanyika ndani ya mwezi huu. Hii ni kwa sababu nimwezi ambao Mtume Muhammadi alionekana akifungasana na kuzidisha ibada. Hivyo sisi kama wafuasi wake tunatakiwa tumfuate kwa vitendo na sio kwa maneno tu.
Kwa wale waliosoma makala yangu iliyopita niliwaelezawazi utukufu wa mwezi huu. Pia niliwahimiza wasomajiwajitahidi kulipa madeni ya swaumu ya Ramadhaniiliyopita kwani tumeagizwa kulipa madeni kabla yakuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
NISFU SHAABANI
NISFU SHAABANI ni usiku wa tarehe 14 kuamkiatarehe 15 Shaabani. Tarehe hii imekuwa ikitukuzwatangia enzi na enzi kuanzia wakati wa maswahabampaka kwa Makhalifa. Baadae emeendelezwa mpakakizazi chetu na inshaallah mpaka siku ya Kiyama.
Nisfu Shaabani, yaani nusu au katikati ya mwezi waShaabani, ni siku ambayo hutumika kama maandalizi yakujiandaa na Ramadhani. Pia ndio hesabu za mjaurufaishwa (upandishwa) kwa Mwenyezi Mungu (S.W) kama alivyosema Mtume Muhammad (S.A.W) na hapaanasimulia Usama Ibn Zaid (RA): “Nilisema ewe Mjumbe wa Allah sikukuona ukifunga katika mweziwowote katika miezi kama siku unazofunga katikamwezi wa Shaaban? Akasema Mtume (S.A.W) …. huoni mwezi ambao watu wameghaflika nao baina ya Rajab na Ramadhan, nao ni mwezi ambao (hurufaishwa) hupandishwa ndani yake amali za watu kwa Bwana waViumbe na napenda zipandishwe amali zangu na hali nimwenye kufunga.” (An-nasai).
Maneno hayo ya Mtume yanaonyesha wazi mwezi huuni muhimu kujiandaa nao. Kuna uhakika kupandishwakwa amali za waja zinazofanyika katikati ya mwezi huu. Hii inatokana na Muadhi bin Jabal akimsikia MtumeMuhammad (S.A.W) akisema kuwa Mwenyezi Mungu(S.W) anawaangalia waja kila usiku wa laylatu nnisfshaban anawasamehe viumbe wake wote isipokuawashirikina na yule mtu mwenye chuki (Twabrani naIbn Hibban na wengineo).
Wenzetu waliotangulia wameutukuza usiku huu hivyo nasisi tuufanyie jitihada na vyema ukakutwa siku hiyoumefunga. Katika vitabu vingi usiku huu umeelezwanamna ya kuupokea na kuadhimisha kwa nia yakupupia ibada ili kupata thawabu za kukuokoa naadhabu za moto wa jahannamu.
Sheikh mkubwa katika uislamu, Ibnu Taimia amesema: “… na usiku wa nisfu Shaaban hakika zimekuja fadhilana ubora wake katika hadith nyingi ….. na maswahabawalikuwa wakiswali ndani yake”. Na hapa tunapatakuwa ni usiku mtukufu (Majumulfatawa). Ukiangaliamasheikh wameendelea kusema kuwa ni vyema kusalipamoja au peke yako usiku huo kwani wamefanyabaadhi ya wakubwa zetu katika uislamu. Imamu Shafiianasema kuwa hakika dua zakubaliwa katika usiku wanisfu shaaban. Baadhi ya maeneo, wenye nafasihukusanyika na kuswali pamoja huku wakipeanamawaidha na kumswalia Mtume Muhammad (S.A.W). Pia ni nafasi ya kuomba dua ya mwisho mwema, dua yakumuomba atufikishe salama katika Mwezi Mtukufu waRamadhani pia na kuomba dua ya mambo yetutuliyonayo ya kila siku. Sisi kama wanaadamu niwahitajia wa kila sekunde kwa Mwenyezi Mungu (S.W).
Kwa maelezo hayo hapo juu, ni vyema kundeleakufanya ibada kwa wingi ndani ya mwezi huu kwanitutapata thawabu nyingi, utajiandaa na Mwezi Mtukufuwa Ramadhani na kujiweka mbali na moto. Mwanadamuamekuwa akitafuta sababu zisizokuwa za msingi iliasifanye ibada. Utamkuta mtu anawatangazia watuwasifanye ibada kumbe anataka afuatwe katikakutomuabudu Mwenyezi Mungu (S.W) na kumswaliaMtume Muhammadi (S.A.W). Mwenyezi Mungu (S.W)anatutaka tuelekezane katika mema na taqwa, na katikakufanya ibada ndogondogo na kubwa ndiokinachokomaza imani na kuzoea kukimbilia kuzifanyaibada. Muislamu yeyote akipata nafasi asiiache hatakidogo kwani hiyo ndio inaweza kumuokoa na majangaaliyonayo na ikamfanya alipwe pepo (Amiina).
MWISHO:
Waislamu wa miji hii na wale wote waliokuja katikaibada ya Umra wanazitumia fursa zote wakiwepo hapa. Nimeona wakikesha usiku misikitini, wakiswali sunna zawitri, na wanakuwa na dua za kuombea nchi zilizokokatika vita ya wenyewe kwa wenyewe au nchi na nchi, wanaitumia vizuri siku ya Akhamisi kwa kufunga nakusimama usiku wake. Nawashauri waamini woteambao hawakujaliwa kuwa katika Miji hii Mitakatifuwaendelea kutekeleza ibada hii.
Swed Twaibu Swed
Mwenyekiti Mtendaji
Tanzania Charitable and Development Organization(TCDO)
Simu 0754 823 461/ 0784 270 290
Email swedtwaibu@yahoo.com