WAZIRI KITWANGA ASIMAMISHWA KAZI RASMI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga
kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.Rais Magufuli ametengua uteuzi huo
kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na
kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.