BHARTI AIRTEL YAKUBALI SERIKALI YA TANZANIA IWE MMILIKI WA HISA ZOTE ZA TTCL
Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel
Afrika Bwana Christian Manuel De Faria (aliyekaa katikati) na Bwana
Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina ( aliyekaa wa kwanza kushoto)
wakiweka saini ya kuiwezesha
Serikali kumiliki hisa za TTCL kwa asilimia 100. aliyesimama nyuma
katikati kuhuhudia ni Dkt. Maria Sasabo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Hafla hiyo ya kuwekeana saini na iliyofanyika
katika ofisi za TTCL Samora jijini Dar es Salaam leo.
Msajili wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru, akionyesha cheti cha makubaliano ya umiliki wa hisa asilimia 35 za Bharti Airtel walizokuwa wakimiliki ndani ya TTCL kwenda serikalini mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel bwana Christian De Faria (kulia) kusainimakubaliano hayo leo.
Picha ya pamoja ni uongozi wa Bharti Airtel na baadhi ya viongozi wa serikali mara baada ya kuwekeana saini ya makubaliano ya umiliki wa hisa asilimia 35 za Bharti Airtel walizokuwa wakimiliki ndani ya TTCL kwenda serikalini.

Dar es salaam 24th Juni 2016
Tanzania, Kampuni ya Mawasiliano
ya simu za mkononi ya Bharti Airtel Leo wamesaini na kuingia
makubaliano ya kuachia hisa zao 35% walizokuwa wakimiliki katika kampuni
ya mawasiliano nchini Tanzania TTCL ili serikali
iweze kumiliki kampuni hiyo ya TTCL kwa asilimia 100.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria
“Bharti Airtel tunaishukuru sana
serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri tuliokuwa nao kwa miaka
mingi kapitia shirika la Tanzania Telecomunication Company Limited
(TTCL).
Bharti Airtel
tunatambua mikakati na nia ya serikali kutaka kuwa mmiliki pekee katika
shirika la TTCL. kutokana na utaratibu na jitihada zenye maamuzi ya
busara toka pande zote Bharti Airtel na Serikali swala
hili limefikia tamati.
Hivyo kwa kumalizika
vyema kwa swala hili la kuirudishia serikali hisa 35% zilizokuwa
zinamilikiwa na Bharti Airtel ndani ya TTCL, Bharti Airtel
tunawakikishia watanzania kwa ujumla kuwa tutaendelea na
mikakati bora ya uwekezaji kati yetu na serikali kupitia Airtel
Tanzania ambapo Bharti Airtel ni mmiliki wa hisa 60%”. alimaliza kusema
De Faria