Bukobawadau

*WAKATI MWINGINE KATIKA MAISHA*

Unahitaji watu watakaokudharau ili ukimbilie kwa Mungu. Unahitaji watu watakaokunyanyasa ili uwe shupavu. Unahitaji watu watakaokwambia HAPANA ili ujifunze kujitegemea au ujifunze namna ya kutatua changamoto zako mwenyewe.
Wakati mwingine unahitaji watu wako wa karibu kabisa ambao hukutegemea siku moja watakuacha, na wakuangushe kipindi ulichowahitaji kuliko chote ili ujifunze KUMWAMINI MUNGU na sio mwanadamu.
Unahitaji BOSS katili atakayekufukuzisha kazi ili uwe na ujasiri wa kuanzisha biashara yako kabla hujazeeka. Unahitaji ndugu watakaokuuza katika nchi ya ugenini ili ukawe waziri mkuu huko Misri (Kama Yusuph).
Unamuhitaji baba mwenye nyumba katili mnyanyasaji na anayepandisha kodi kila mwezi ili ujifunze kujenga yako mwenyewe na ikimalizika uiheshimu na uheshimu wenzio waliojenga.
*KWA KIFUPI TAMBUA KUWA*
Kila jaribu huambatana na baraka zake, wakati mwingine huwezi kuona baraka Mungu anazokufungulia katika mlango mwingine huku ukiwa umeshupalia kusukuma mlango ambao Mungu amaeufunga.
*MUHIMU*
Tambua kuwa hakuna jaribu ama dhihaka inayokuja kwako bila kuwa na baraka nyuma yake. Ndugu zangu upatapo jaribu lolote juwa linaambatana na baraka, muombe Mungu akupe macho na uvumilivu wa kuona BARAKA zake pale upatapo na jaribu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau