Bukobawadau

BENKI YA POSTA YAPATA FAIDA YA SH BILIONI 8.84 KABLA YA KODI KWA NUSU YA KWANZA YA MWAKA 2016

Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
***********
NUSU ya kwanza ya Mwaka 2016 iliyoisha mwezi Juni, imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Pamoja na changamoto mbalimbali ambazo bado zinaikabili benki yetu, kwa kipindi kirefu sasa, lakini Benki imefanikiwa kupata faida kabla ya kodi ya shilling bilioni 8.84 ukilinganisha  shillingi bilioni 5.48  zilizopatikana kipindi kama hicho mwaka 2015,ambayo ni sawasawa na ukuaji wa asilimia 61.47%. 



Ukuaji huu wa faida katika kipindi hiki cha nusu mwaka wa 2016 umewezesha kukua kwa mtaji wa wawekezaji hadi kufikia shillingi billioni 48 kutoka shillingi bilioni 37 mwezi Juni mwaka 2015.

Mapato ya Benki kwa nusu mwaka 2016 yaliongezeka hadi kufikia shilling bilioni 42.5 kutoka bilion 34 iliyofikiwa nusu ya mwaka 2015, huu ni  ukuaji wa asilimia 38%. Vilevile katika kipindi hichohicho amana za wateja ziliongezeka na kufikia shilingi bilioni 294.64 kutoka shilingi bilioni 263.68 June mwaka 2015, ukuaji wa asilimia 11.74%.

Mikopo imeongezeka hadi kufikia shillingi billioni 278 kutoka shilingi billioni 241.51 Juni mwaka 2015, ongezeko la asilimia 15.22%. Sehemu kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na wafanyakazi wa sekta  ya umma na serikali kuu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Rasilimali za benki zilikuwa hadi kufikia shilling 390.8 bilioni mwezi Juni mwaka huu 2016 kutoka shillingi billioni 333.96 Juni mwaka 2015 ongezeko la asilimia 17.16%.

Benki ya Posta kwa mwaka 2016, iliendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, ambapo Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Msajili wa Hazina Bw.Lawrence Mafuru. 

Matawi hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Benki ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama. 

Pia, benki imehamisha tawi lake la Moshi kwenda kwenye jengo jipya la NSSF, na hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya kisasa zaidi.

Hadi hivi sasa TPB inayo matawi 30 na madogo (min branches) 30, Mashine za kutolea pesa (ATM) zinazo milikiwa na benki ya posta ni 38 na 200 za umoja wamabenki (Umoja switch), hivyo kuwawezesha wateja wetu kupata huduma ya pesa nchi nzima.

Pia benki inao mawakala wa benki 133 kupitia TPC,na vituo vya huduma 200 kupitia mawakala binafsi.

Benki ya posta inaendelea na jitihada zake za kuongeza wigo wa biashara kwa njia mbalimbali, zikiwemo:

kutoa  mikopo kwa vikundi vidogo vidogo  (group lending), ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 6.5 bilioni na huduma ya  kuwakopesha wazee (wastaafu loan) kupitia mifuko ya jamii  kama vile  PSPF,NSSF na ZFF, ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 56 bilioni.

Kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), enki imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 541 ili kuviinua kiuchumi vikundi vilivyo chini ya Baraza hilo.

Kufungua account za vikundi visivyo rasmi(VICOBA informal groups) ambapo hadi sasa akaunti 30 elfu zimefunguliwa.

Huduma za kibenki  kupitia simu za kiganjani,ambapo kwa kipindi cha nusu ya mwaka huu akaunti 271,427 zilifunguliwa, kulinganisha na akaunti 236,981 zilizofunguliwa hadi mwishoni mwa mwaka jana. Hili ni ongezeko la akaunti 34,446, sawasawa na asilimia 15.      
                                
Benki ya Posta imejidhatiti kuendelea kutoa huduma bora, nafuu na za kisasa kwa maana ya kutumia teknolojia zaidi katika kipindi hiki. Tunaamini kwamba bado kwa kutumia teknolojia ya TPB POPOTE tutaweza kuwafikia Watanzania walio wengi hasa vijijini ambao bado hawajaingia kwenye mfumo wa kifedha.

Pia benki itaendeleza na kuboresha mahusiano yake na makampuni za simu ili kuweza kupeleka huduma zake karibu zaidi na wananchi, na pia ushirikano wake na Saccos pamoja na Vicoba.

Benki ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama nafuu.

Pia shukrani za pekee ziende kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa uongozi wao thabiti na usimamizi imara, unaoendelea kuhakikisha kuwa benki inakuwa miongoni mwa taasisi bora za kifedha hapa nchini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau