DC BUHIGWE ATOA SIKU SABA KUKAMILISHA MFUMO WA NYUMBA KUMI ZA KIUSALAMA
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti.
*******
*******
MKUU Wa Wilaya ya Buhigwe,
Mkoani Kigoma, Col Marco Gaguti amewataka Viongozi wa Serekali na jamii
Wilayani Buhigwe kuwatumikia Wanachi kwa nguvu zote na kuhakikisha uundwaji wa
mfumo wa nyumba kumi.
Aidha Viongozi hao wa Serikali
na jamii wametakiwa kukamilisha mara moja uundwaji wa mfumo wa kiutawala wa
nyumba kumi ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na amnani katika wilaya hiyo.
“Ninatoa siku saba kukamilisha
zoezi la kuhuisha daftari la kiusalama pamoja na uundwaji wa mfumo wa kiutawala
wa nyumba kumi ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa cha ulinzi na usalama wetu,”alisema
Col. Gaguti.
Col Gaguti alibainisha hayo
alipokuwa akiongea na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja
na Viongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya katika kikao cha kujitambulisha
kilichofanyika Julai 11,2016 katika ukumbi Wa Mikutano Wa Wilaya.
" Nataka kila Kiongozi
ajipambambanue kwa kuwapigania na kuwatumikia wanachi,niwakati sasa wa kila
mmoja wetu kuainisha kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa
haraka," alisema Col Gaguti.
Amewataka kuweka kipaumbele
katika kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati ya kushughulikia kero za
wananchi.
Col Gaguti alisema watendaji wa serikali kila ngazi wasimamie
vyema shughuli za serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha lego la Serekali
kutoa elimu bure yenye ubora lifikiwa mapema kwa kukamilisha mahitaji yote
muhimu na kusimamia huduma bora za Afya
.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimia baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Hlamashauri kwaajil;i ya kikao cha kujitambulisha.Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimia baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Hlamashauri kwaajil;i ya kikao cha kujitambulisha.
Akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya
watumishi wakimsikiliza mkuu huyo wa Wilaya. Source:Father Kidevu Blog