Bukobawadau

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. --- Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi. Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.  Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu. --- Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development. Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu. Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 
Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza. --- Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza. Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu. "Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba," alisema mkurugenzi huyo na kuendelea: Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa. Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao. Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.  
Next Post Previous Post
Bukobawadau