Bukobawadau

TAARIFA YA MADAWATI KATIKA MKOA WA KAGERA KUFIKIA TAREHE 30 JUNI, 2O16

Ndugu Waandishi wa Habari, apenda nichukue fursa hii kupitia kwenu na vyombo vyenu vya habari kuwajulisha umma wa wananchi wa Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla jinsi mkoa wetu ulivyotekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli alilolitoa wakati akituapisha Wakuu wa Mikoa alipoagiza kuwa ifikapo Juni 30, 2016 asiwepo mwanafunzi anayekaa chini katika shule za Msingi na Sekondari.
 Ndugu Waandishi wa Habari, kwa Mkoa wetu wa Kagera katika ELIMU YA MSINGI madawati yanayohitajika ni 200,439 Madawati yaliyokuwepo kabla ya agizo ni 135,838 Madawati ambayo yametengenezwa tangu agizo kutolewa ni 30,960 Jumla ya madawati yaliyokuwepo awali na yaliyotengenezwa baada ya agizo kutolewa ni 176, 877 ambayo ni sawa na asilimia 88%. Aidha upungufu ni madawati 23,806 ambayo ni sawa na asilimia 12%.
 Ndugu Waandishi wa Habari, kwa Mkoa wetu wa Kagera katika ELIMU YA SEKONDARI madawati yanayohitajika ni 72,105 Madawati yaliyokuwepo kabla ya agizo kutolewa ni 62,832 Madawati ambayo yametengenezwa tangu agizo kutolewa ni 4,996 Jumla ya madawati yaliyokuwepo awali na yaliyotengenezwa baada ya agizo kutolewa ni 68,907 ambayo ni sawa na asilimia 96%. Aidha upungufu ni madawati 3,198 ambayo ni sawa na asilimia 4%.
 Ndugu Waandishi wa Habari, nawapongeza wananchi wote wa Mkoa wa Kagera, Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali, Watu Binafsi pia na Makampuni mbalimbali yaliyoguswa na kuchangia madawati katika mkoa wetu. Aidha naendelea kuhamasisha kila mwananchi au Taasisi itakayoguswa na suala hili la uchangiaji wa madawati kuendelea kuchangia ili tumalize tatizo la watoto wetu kukaa chini ili wapate elimu iliyobora katika mazingira rafiki ya kujifunzia.
 Ndugu Waandishi wa Habari, baadhi ya changamoto zilizochangia kutokamilika utengenezaji wa madawati kwa wakati ni pamoja na:-
• Kulikuwa na Tafsiri duni ya dhana ya Elimu bila malipo ambapo mwanzoni wananchi walisuasua kuchangia.
• Muda mwingi ulipotea wakati wa kusubiri mbao kukauka
• Kutokuwa na umeme wa uhakika kwani madawati mengi yanatengenezwa kwa fremu za chuma katika wilaya ya Ngara.

Hata hivyo Halmashauri ambazo hazijakamilisha utengenezaji wa madawati zitakamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe 30 Julai, 2016.
Imetolewa na; Mhe. Meja Jenerali (Mst) Salum M. Kijuu
Mkuu wa Mkoa Kagera.
Next Post Previous Post
Bukobawadau