WAZIRI MWAKYEMBE AAGIZA KAMATI ZA MAADILI YA MAHAKIMU KUANZISHWA MARA MOJA MKOANI KAGERA ILI KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (kulia) Akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Salum M. Kijuu.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Akiongoza Msafara kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
Meza Kuu Wakiimba Wimbo wa Hamasa wa Mkoa wa Kagera
Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini Akichangia Jambo
Ukumbi Mzima Ukiimba Wimbo wa Hamasa
Waziri Mwakyembe Akiteta Jabmbo na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini Bw. Biswalo Mganga
Waziri Mwakyembe Akigawa Vyeti kwa Wananchi waliokuja kupokea vyeti vyao baada ya kujiandikisha
Picha ya Pamoja Waziri na Uongozi wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Akiongoza Msafara kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
Meza Kuu Wakiimba Wimbo wa Hamasa wa Mkoa wa Kagera
Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini Akichangia Jambo
Ukumbi Mzima Ukiimba Wimbo wa Hamasa
Waziri Mwakyembe Akiteta Jabmbo na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini Bw. Biswalo Mganga
Waziri Mwakyembe Akigawa Vyeti kwa Wananchi waliokuja kupokea vyeti vyao baada ya kujiandikisha
Picha ya Pamoja Waziri na Uongozi wa Mkoa.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt
Harrison Mwakyembe aliyasema hayo wakati akiongea na wadau mbalimbali waliopo
chini ya Wizara yake, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Waandishi wa Habari, Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Mhe. Salum M. Kijuu
katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kagera alipowasili Mkoani Kagera leo tarehe
14/07/2016 na kuanza ziara yake ya kazi ya siku tatu.
Waziri Mwakyembe aliyeongozana na
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Bw. Biswalo Mganga na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
RITA Bi Emmy K. Hadson alisema katika kikao hicho kuwa ziara yake mkoani
Kagera inalenga mambo makuu matatu kama ifuatavyo;
Kwanza ni kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sheria iliyonzishwa mwaka 2011ambayo
ilianzisha Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo ndani yake ilianzisha Kamati za
Maadili ya Mahakimu wa Mahakama za mwanzo katika ngazi ya Wilaya na Kamati za
Maadili ya Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Wilaya katika ngazi ya Mkoa.
Katika kuhimiza utekelezaji wa
sheria hiyo Waziri Mwakyembe aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kuunda Kamati hizo ili
kutatua kero za wananchi wanazopata kutoka Makimu wa Mahakama za Mwanzo ambao
wanajifanya miungu watu na kuwanyanyasa wananchi kwa kuwaomba rushwa na
kupindisha haki. Aidha alimwagiza Mkuu wa Mkoa naye kuunda kamati hiyo ya mkoa
ili kutatua kero za malalamiko kwa Mahakimu Wakazi na Makimu wa Wilaya.
Kamati hizo za Maadili katika
ngazi ya Wilaya wajumbe wake ni Mkuu wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ni katibu wa kamati hiyo, Mkuu wa Wilaya pia
atateua kiongozi mmoja katika Wilaya husika na Mwananchi mmoja anayeheshimika
katika jamii nao watakuwa wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Hakimu Mfawidhi wa
Wilaya naye ni Mjumbe.
Pili, Waziri Mwakyembe alisema katika ziara yake Mkoani Kagera ni
kuhimiza juu ya uchukuaji na utunzaji wa takwimu za vizazi na vifo hasa
kwa watoto wadogo. Waziri Mwakymbe
alisema kwa nchi nzima ya Tanzania uandikishaji wa takwimu za vizazi na vifo bado
ni tatizo kubwa kwani katika Tanzania watoto na watu wazima takwimu zinaonyesha
kuwa wenye vyeti vya kuzaliwa nia asilimia 11% tu.
“Tatizo lilionekana kuwa kubwa
baada ya Serikali kuamua kutoa elimu bure hapo ndipo ilionekana kuwa mfumo wetu
wa takwimu una matatizo makubwa kwani watoto
walifumuka sana kiasi ambacho hapo awali takwimu zilikuwa hazioneshi kuwa
wtotot hao wapo katika jamii.” Alisistiza Mhe. Mwakyembe.
Aidha Waziri Mwakyembe aliushukuru
uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kuvuka asilimia ya kitaifa kwa uandikishaji wa
vizazi na vifo kwani kwa Mkoa ni
asilimia 12% ambapo kitaifa ni asilimia 11% na Wilaya ya Bukoba inaongoza kwa
asilimia 45%, Wilaya ya mwisho ni Kyerwa ambayo kwasasa imeandikisha asilimia 9.4%
Angalizo, Waziri Mwakyembe pamoja na kuushukuru uongozi wa Mkoa na
kumuomba Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya
kuongeza juhudi za uhamasishaji wa wananchi kuona umuhimu wa kuandikisha watoto
wao lakini alitoa angalizo kuwa Mkoa lazima kuwa makini sana katika uandikishaji
huo ili kudhibiti wahamiaji toka nje ya nchi kuandikishwa .
Tatu, Waziri Mwakyembe alisema amekuja Mkoani Kagera kuona tatizo
la mlundikano wa Wafungwa na mahabusu Magerezani
ambapo alisema kuwa amekuwa akitembelea Magereza kila Mkoa alipofanya ziara ili
kuona ukubwa wa tatizo ni kiasi gani na kuona jinsi ya kutatua changamoto hiyo
Wizara yake ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa badala
ya kuongea na raia juu ya tatizo la mlundikano wa wafungwa yeye akishirikiana
na Waziri wa Mambo ya Ndani waliamua waongee na wafungwa ili kujua tatizo kwa
undani na katika kuongea na wafungwa hao katika Magereza mbalimbali nchini
waligundua yafuatayo:
Ucheleweshwaji wa nakala za
hukumu za kesi, jamabo ambalo tayari Mahakama
tayari zimeanza kulishughulikia kwa kasi
kubwa, pili Kesi za watuhumiwa kukaa
muda mrefu bila kusikilizwa, nalo pia mahakama imeanza kulishughulikia, na Tatu
Watuhumiwa kubambikiziwa kesi tofauti na kesi zilizowapeleka Magereza. Waziri
Mwakembe alisema matatzo yote hayo sasa yanashughulikiwa kwa kasi kubwa sana na
Mahakama.
Aidha, katika hatua nyingine Mhe.
Mwakyembe alitembelea Ofisi ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)
katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba na kumuagiza Kaimu Mtendaji Mkuu
kuhaikikisha anaiwezesha ofisi hiyo vifaa vya kisasa kama (Kompyuta) ili
kurahisisha utendaji kazi kwani Wilaya hiyo imepiga hatua kubwa katika
uandikishaji, vile vile aligawa vyeti vya kuzaliwa kwa wanaume watano na
wanawake watano.
Waziri Mwakyembe atakuwepo Mkoani
Kagera kwa siku tatu tarehe 14-16/07/2016 na anatarajia kutembelea Mahakama
kuu, Gereza la Mkoa Bukoba, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Gereza la Wilaya ya Muleba na Gereza la Wilaya ya Biharamulo
na kuhitimisha ziara yake Wilayani humo.