MKUU WA MKOA WA KAGERA AWAAGIZA VIONGOZI MKOANI HUMO KUSIMAMIA HUDUMA ZA AFYA KIKAMILIFU
MKUU WA MKOA WA KAGERA
AWAAGIZA VIONGOZI MKOANI HUMO KUSIMAMIA HUDUMA ZA AFYA KIKAMILIFU
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja
Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu awaagiza viongozi katika Halmashauri za Wilaya
kuchukukua jukumu la kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali za afya
katika Mkao wa Kagera ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kikamilifu
katika jamii.
Mhe. Kijuu alitoa agizo hilo
wakati akifungua kikao cha wadau wa afya Agosti 23, 2016 katika Ukumbi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Kagera kilichowahusisha
Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na
Wadau mbalimbali wa Serikali na wasiokuwa wa Serikali wanaoshirikiana katika
kutoa huduma mbalimbali za afya Kagera.
Katika Agizo hilo Mkuu wa Mkoa
alisistiza mambo makuu na muhimu matatu kama ifuatavyo; Kwanza aliwaagiza
viongozi hao kuhakikisha wanajadili kwa kina na kuweka mikakati ya kutoa huduma
ya chanjo katika Halmashauri za Wilaya
ili ziweze kufikia asilimia 95% ya Kitaifa .
Pili ni kuhakikisha viongozi
wanapitishwa na kuelimishwa kwa undani zaidi na wataalamu wa afya kuhusu vigezo
vilivyotolewa na wafadhili wanaotoa fedha za Busket Fundi ili
kushirikiana katika usimamizi kwenye Halmashauri za Wilaya kukamilisha mahitaji
ya vigezo hivyo ili zikidhi vigezo hivyo na kupata fedha za wafadhili zikawahudumie
wananchi kupitia sekta ya afya.
Mhe. Kijuu alisema kuwa katika
majaribio ya awali yaliyofanyika katika kutathmini vigezo hivyo ilionyesha kuwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ilipata asilimia 93%, Muleba 83%, Bukoba 14% aidha
Biharamulo ilipata asilimia 0% (sifuri) na Halmashauri nyingine kutokana na wataalam
wa afya kutoingiza takwimu za afya katika mfumo wa Wizara ya Afya , Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Mhe. Kijuu pia aliwakumbusha
viongozi hao kuhakikisha wanasimamia na kuchukua tahadhali zote juu ya
kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo aliagiza vituo vyote vya afya hapa Mkoani
Kagera kuanza kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa Halmashauri za Wilaya ambazo hazijaanza
kutoa huduma hiyo zianze mara moja, pia kuimarisha Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF)
ili kupata fedha za tele kwa tele.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dk. Thomas Rutachunzibwa
aliwashukuru wadau wote wa afya wa Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Serikali
katika kuhakikisha huduma za afya Mkoani Kagera zinaimarika na aliwaomba
kuendelea na ushirikiano wao mzuri ili kuboresha afya za wananchi wa Mkoa wa
Kagera .