MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AFANYA ZIARA YA KUSHUTUKIZA KATIKA MRADI WA MAJI KUONA KAMA ALIUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA WATENDAJI
Mhe. Kinawilo wa2AA Pili Akiongozwa na Mhandisi Mtagaywa wa Kwenda Kuhakiki Tenki la Maji Juu.
Mhe. Kinawilo (wa pili kutoka kulia) aliyeshika Viungio vya Maji Akimhoji Bw. Dismas Martin Juu ya Ubora wa Viungio vya Mabomba.
Mhe. Kinawilo Akiwahoji Diwani wa Kata Nyakibimbili Mwenye Baragashia Haji M. Juma na Anayefuata Mwenyekiti wa Kijiji Kitahya Bw J. Kahigwa.JPG
Tanki Dogo Linalokusanya Maji Katika Chanzo
Mhandisi Mshauri Mwesigwa Mtagaywa aliyeinama Akimwonyesha Mhe. Kinawilo Mabomba Yaliyokatwa na Wananchi kama hujuma ya Miundombinu ya Mradi.
Mhe. Deodatus Kinawilo (wa pili kutoka kushoto waliosimama juu ya Tenki) Mara Baada ya Kuhakiki kuwa Pampu Imo ndani ya Tenki
Tanki Dogo Linalokusanya Maji Katika Chanzo.
Mhe. Kinawilo (wa pili kutoka kulia) aliyeshika Viungio vya Maji Akimhoji Bw. Dismas Martin Juu ya Ubora wa Viungio vya Mabomba.
Mhe. Kinawilo Akiwahoji Diwani wa Kata Nyakibimbili Mwenye Baragashia Haji M. Juma na Anayefuata Mwenyekiti wa Kijiji Kitahya Bw J. Kahigwa.JPG
Tanki Dogo Linalokusanya Maji Katika Chanzo
Mhandisi Mshauri Mwesigwa Mtagaywa aliyeinama Akimwonyesha Mhe. Kinawilo Mabomba Yaliyokatwa na Wananchi kama hujuma ya Miundombinu ya Mradi.
Mhe. Deodatus Kinawilo (wa pili kutoka kushoto waliosimama juu ya Tenki) Mara Baada ya Kuhakiki kuwa Pampu Imo ndani ya Tenki
Tanki Dogo Linalokusanya Maji Katika Chanzo.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe.
Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza katika Kata Nyakibimbili Kijijini
Kitahya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba leo Agosti 9, 2016 katika chanzo cha
maji kilichopo kijijini hapo ili kuhakiki kama pampu ya kusukuma maji kama ilifungwa na ipo katika tenki la maji
lilojengwa katika chanzo hicho cha maji.
Mkuu huyo wa Wilaya aliamua
kufanya ziara hiyo ya ghafla na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama mara baada ya
kuletewa malalamiko na wananchi kuwa siku mradi huo ulipowekewa jiwe la msingi
na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. George Mbijima Julai 27, 2016 maji
yaliyotoka katika ghati la Ibwera yalijazwa kwenye tenki na gari la kubebea
maji kwani pampu ya kusukuma maji
haikuwepo katika tenki lilipo kwenye chanzo cha maji.
Baada ya kufika katika chanzo
hicho cha maji Mhe. Kinawilo aliyeongozana pia na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bw. Gregory
Fabian, Mhandisi wa Maji Bw. Dismas
Martin, na Mhandisi Mshauri wa Mradi huo Mwesiagwa Mtagaywa wa Kampuni ya (O
& A Company Ltd.) alikagua mradi huo na kugundua kuwa pampu ipo na inafanya
kazi vizuri ya kusukuma maji.
Aidha, iligundundulika kuwa maji
mara baada ya kusukumwa kutoka kwenye
tenki umbali wa mita 22 kutoka kwenye
tenki hilo bomba limekatika kiungio jambo linalosababisha maji kutopanda hadi
katika Kata ya Ibwera ambapo Mhe. Kinawilo alimuagiza Mhandisi Mshauri
kuhakikisha anamshauri Mkandarasi kufanya marekebisho ya haraka nadani ya wiki
moja.
Aidha , katika mradi huo
kuliibuliwa suala la wananchi kukata mabomba ya maji katika chanzo hicho na
kusababisha maji kutoenda katika tenki linalohudumia vijiji vitatu vya Kitahya,
Kibona na Itongo na kusababisha Diwani wa Kata ya Nyakimbimbili Haji Matsawilly
Juma kulalamika kuwa maji hayawafikii wananchi na kumwomba Mkuu wa Wilaya
kumhimiza Mkandarasi kumaliza kazi ili maji yatoke kwa wananchi kama
ilivyotarajiwa.
Maagizo, Mhe. Kinawilo baada ya kushuhudia uharibifu huo alimwagiza
Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anafunga vifaa vyenye ubora ili thamani
ya vifaa iendane na gharama za mraddi huo. Pili alimwagiza Mwenyekiti wa Kijiji
Kitaya Bw.Johnstone Kahigwa aliyedai
kuwa kijiji hakikukishirikishwa tangu mwanzo wa mradi kuhakikisha anashirikiana
na Halmashauri ya kijiji chake kuilinda miundombinu ya mradi huo kwa sababu
mradi upo katika eneo lake.
Vilevile Mhe. Kinawilo alimwagiza
Mhandisi Mshauri kuhikikisha anfanya marekebisho yote ya mradi huo ndani ya
wiki moja ili wananchi waanze kupata huduma ya maji. Na mwisho aliwaagiza
Watendaji wa Kata za Ibwera na Nyakibimbili kuititsha mkutabno wa pamoja kwa
kamati za maji za Vijiji vya Kitaya, Kibona,Itongo na Ibwera ili kuweka
mikakati ya kuilinda miundombinu ya mradi huo wa maji.
Mradi huo wa maji ukikamilika
unatarajiwa kuhudumia vijiji vinne vya Kitaya, Kibona,Itongo (Kata Nyakibimbili)na Ibwera (kata Ibwera)
una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 430 na ulianza katika awamu ya kwanza
mwaka 2009 katika upembuzi yakinifu na usanifu, aidha utekelezwaji wake ulianza
rasmi katika awamu ya pili iliyoanza
Mwezi Julai, 2013.