SHIDA KUBWA YA MAJI WILAYANI KARAGWE!!
Ukweli ni kwamba ukiwa nje ya wilaya hii ya Karagwe hutawaza kwamba kuna uwezekano wa kuwepo tatizo la maji la kiasi hiki katika maeneo mengi na Mji wa Kayanga ambao ndio makao makuu ya Wilaya yenye majimbo mawili makubwa ya Karagwe na Kyerwa
Foleni kubwa ya wananchi wakati wakisubilia huduma ya maji maeneo ya Omulushaka Karagwe
Pichani wanaonekana Wakazi wa kijiji cha Kiyanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutoka katika shimo lilochimbwa bondeni ,na hiki ndicho chanzo kikubwa wanachokitegemea pamoja na kwamba maji hayo ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea kunyesha kwa mvua sio salama kwa binadamu,wakiongea na mwanalibeneke wetu Wakazi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji hayo hayo.
Kadhia hii ya maji ni alama mbaya sana kwa wazawa wote wa Karagwe waishio ndani na nje ya Wilaya ya hii pia ni aibu na alama kubwa ya usaliti wa wawakilishi wao wote wa vipindi mbalimbali!!
Hakika
ni lazima zitumike nguvu za ziada kuwaokoa wananchi hawa wanaokatiza
usingizi kila siku kwenda kupanga foleni ya maji katikati vyanzo
mbalimbali.
Credit Photo:@Mc Baraka