BODI YA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM YAJIUZULU.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Bodi ya Uhuru Media Group
inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru
Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na
Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha
kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj
Adam O. Kimbisa.
Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt
John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe
22 Septemba 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote
wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.
Bodi ya Uhuru Media Group
ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia, kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti
ya Makampuni hayo na kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza ufanisi katika
uendeshaji wa vyombo vya habari vya Chama.
Imetolewa na:-
CHRISTOPHER
OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI
WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe
22/09/2016.