CHANGAMOTO YA MAKAZI #TETEMEKOBUKOBA!!
Kilio cha Mwanamama Yasinta Silvesta (pichani katikati) mkazi Hamugembe- Kashabo ambaye
nyumba yake yenye vyumba 7 ilibomomoka baada ya Jiwe kubwa (Jabali)lililong'oka
na kuangukia nyumba hiyo kufutia tukio la #TetemekoBukoba
Yeye mwenyewe na baadhi ya waathitika Majirani wanaomba Serikali impatie msaada wa haraka pia wadau mnaweza kumsaidia chochote
Yeye mwenyewe na baadhi ya waathitika Majirani wanaomba Serikali impatie msaada wa haraka pia wadau mnaweza kumsaidia chochote
Shukrani kwa msaada wa awali kutokea kwa Mdau Mwesiga Kyaruzi aliyeweza kutoa msaada wa Godoro,blanketi,na Chakula.
Kabla camera yetu kufika mitaa hiyo, Mama huyo anasema msaada pekee uliomfikia mapema ni hilo turubai moja kutoka (RedCross) lililojengwa kibanda cha kupumzikia ,Mpaka sasa Maafisa wa serikali katika eneo hili bado wanaendelea
kutathmini maafa yaliyosababishwa na tetemeko hilo la ukubwa wa 5.7
kwenye vipimo vya Richter.
Wito kwa Msamalia mwema yoyote anayetaka pia kumsaidia anaweza kumpata kupitia namba zake 0753 611 206 ama kupitia uongozi wa Serikali ya Mtaa ya Hamugembe
Picha ya juu inaonyesha Godoro na vifaa vingine vya ndani vikiwa vimefukiwa na Udongo ,Mpaka sasa Mama huyo na Mjane mwenye watoto wanne hawana mahali pa kulala, hawana chakula na vyombo vya ndani #TetemekoBukoba
Ustaadh Suleiman Bengeso Salum pichani, Mkazi wa Kashabo -Hamugembe Bukoba akielezea namna hali ya taaruki ilivyowapata kufutia #TetemekoBukoba Sep 10,2016