DC BUKOBA AONGEA NA BARAZA LA MADIWANI,ATEMBELEA MAENEO YANAYOFANYIWA UKARABATI
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na Baraza la Madiwani la halmashauri ya bukoba na kuwataka kuacha kulalamika hasa katika kipindi hichi cha kurudisha hali ya kawaida baada ya tetemeko la ardhi kutokea bali watafute njia itakayoleta majawabu ya mambo yanayojitokeza.
Baadhi ya Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro wakati wa kikao cha dharura cha baraza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Kashai iliyoripotiwa na moja ya kituo cha televisheni nchini kuwa shule hiyo imefungwa kutokana na athari za tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akiongea na walimu wa shule ya msingi Kashai alipowatembelea ili kuona maendeleo ya wanafunzi baada ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na moja ya kituo cha televisheni nchini kuwa shule hiyo imefungwa kutokana na athari za tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akikagua nyumba za muda za walimu wa shule ya msingi Kaishaza mkoani Kagera baada ya nyumba zao kuathirika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akikagua ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.