HUKO KANYIGO MAELFU WAMZIKA BI ESTHER RWEGASIRA
Hivi ndivyo ilivyokuwa Safari ya Mwisho ya Maisha ya Bi Esther Rwegasira aliyekuwa Mke wa Marehemu Balozi Joseph Rwegasira aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje,na Mbunge wa Nkenge mpaka mwaka 2000.
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Lt.Col.Denis Filangali Mwila akisalimiana na wafiwa mara alipofika msibani hapo kumwakilisha mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambeya ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Lt.Col.Denis Filangali Mwila pichani kulia akitoa mkono wa pole kwa wafiwa alipofika kushiriki Shughuli ya maziko ya Marehemu Bi Esther Rwegasira yaliyofanyika siku ya Ijumaa nyumbani kwake Kijijini Bukombe Kanyigo
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye ,bi Halima katibu wa Wazazi Wilaya Missenyi na wa mwisho kulia ni Mama Mbae katibu wa CCM wilaya ya Missenyi
Wanaonekana Mamia ya Waombolezaji wakiwa na nyuso zenye huzuni wakati wa shughuli ya Ibada ya Mazisho ya Marehemu Bi Esther Rwegasira .
Julius (Tiba) Rwegasira akiwa amebeba picha ya Marehemu Mama yake mpendwa
Hakika ni Simanzi kubwa kwa wanafamilia na waombolezaji kwa ujumla kufuatia msiba huu mkubwa
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Marehemu Bi Esther Rwegasira
Joanitha na Pamela ambao ni watoto wa kike wa marehemu wakiwa na simanzi kubwa.
Wakati mwili wa Marehemu ukitolewa ndani.
Anaitwa Lutta mtoto wa mwisho wa Marehemu Bi Esther Rwegasira akiweka Msalaba kwenye Jeneza muda mchache kabla ya Ibada maalum kuanza
Bi Juliana Mero mkazi wa Manispaa ya Mji Bukoba ameweza kushiriki shughuli ya maziko ya rafiki yake mpendwa.
Taswira mbalimbali waombolezaji wakiendelea kufuatilia kinachojiri msibani hapa.
Waumini wa Kikatoliki wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mpendwa wetu Esther Rwegasira
Shughuli ya Maziko ya Marehemu Bi Esther Rwegasira yaliyofanyika Nyumbani kwake Kijijini Bugombe-Kanyigo Wilayani Missenyi yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Viongozi wa Vyama na Serikali.
Mamia ya waombolezaji wakiendelea kushiriki Ibada ya Maziko
Ibada ya maziko ikiendelea
Pichani katikati ni Mr.Shuli Mrengo yeye ni mkwe katika familia hii
Umati wa wananchi wa Kiijiji cha Kanyigo na maeneo mengine ya jirani wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuuaga na kuuzika mwili wa Mpendwa wao.
Pichani anaonekani ndugu Essau Kayungi
Umati wa Waombolezaji wakiwa na nyuso zenye uzuni
Moja ya familia iliyoguswa na msiba huu mkubwa ni Mfamilia ya Marehemu Mzee Njunwa wa Kanyigo, pichani kushoto anaonekana Bi Jovitha Njunwa katika hali ya majonzi
Photo Credit @ Mc Baraka
Kushoto pichani anaonekana Mzee Joseph Masabala na kulia kabisa ni Mzee Elias Mashashi
Umati wa maombolezaji wakiendelea na Ibada maalum ya Mazishi ya Bi Esther Rwegasira
Wanakwaya wakiendelea kuimba moja ya nyimbo za kumtukuza Mungu wakati wa shughuli ya mazishi hayo iliyofanyika tarehe 2,9,2016 huko Kijijini Bugombe Kanyigo.
Bw. Hafidh (Nkurukumbi) na Bw. Haruna Goronga pichani wakiwa mamehudhuria maziko hayo
Shughuli ya Ibada ya mazishi hayo ikiongozwa na Fr.Medericus Kyaruzi wa Parokia ya Mugana.
Wanafamilia wakitoa heshima za mwisho kwa Bi Esther Rwegasira
Wanafamilia wakiendelea kushiriki zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao
Mtoto wa Marehemu Bi Esther Rwegasira,pichani ni Jovitha Rwegasira akitoa heshima zake za mwisho kwa mpendwa mama Yake.
Dada Joanitha akitoa heshima zake za mwisho
Watu wakishindwa kabisa kujizuia kutoa machozi ya huzuni wakati wa kutoa heshima zao za mwisho kuaga mwili wa Marehemu Bi Esther Kyaruzi
Poleni sana wote mliofika na msiba huu
Zoezi la kutoa heshima za mwisho likiwa badao linaendelea
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo wakishirikiana na wanafamilia katika kutoa heshima za mwisho kumuaga mpendwa wao
Pole Sana Dada Pamela kwa kuondokewa na mama yako mpendwa
Wanafamilia na waombolezaji kwa pamoja wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho
Fr.Medericus Kyaruzi wa Parokia ya Mugana akinyunyuzia maji ya baraka kwenye Jeneza lenye mwili wa Marehemu Bi Esther Kyaruzi
Fr. Rwiza Matias akiweka maji ya Uzima kwenye Jeneza lenye mwili wa Marehemu Bi Esther Rwegasira
Sehemu ya wadau walioshindikiza mwili wa Marehemu kutoka Jijini Dar es Salaam
Watoto wa Marehemu wakishiriki zoezi la kuweka Udongo
Utaratibu wa kuweka Udongo kwenye kaburi
Eneo la kaburini Shughuli ya Maziko ya Marehemu Bi Esther ikiendelea jioni ya Jana Ijumaa Sep 2,1015
Mr. Shuli Mrengo akiendelea kushiriki mazishi ya mama mkwe wake Marehemu Bi Esther Rwegasira.
Padre wakati wa kusimika msalaba kwenye Kaburi la Mpendwa wetu Ma Esther Rwegasira
Utaratibu wa kuweka mashada ya Maua kwenye Kaburi la Marehemu Bi Esther Rwegasira
Rutta na Tiba ambao ndio watoto wa kiume wa Marehemu Bi Esther Rwegasira wakiweka shada la maua.
Watoto wa kuzaliwa na Marehemu Bi Esther Rwegasira wakati wa utambulisho
Waonekana baadhi ya wanafamilia pichani
Kutoka Kijijini Bugabo pichani ni Kaka wa Marehemu Bi Esther Rwegasira
Kijana Julius (Tiba) Rwegasira akisoma wasifu wa Marehemu Mama yake mzazi Bi Esther Rwegasira
Salaam za rambirambi kutoka kwa Diwani wa Kata ya Kanyigo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Missenye Mh. Tegamaisha akitoa salaa za rambirambi
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Lt.Col.Denis Filangali Mwila akitoa Salaam za rambirambi kwa niaba yake na kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Diwani wa Kata Kashenye(Omulangira)Adeodatus Rugaibula ameweza kushiriki kikamilifu shughuli hii ya maziko iliyofanyika Kijijini Bugombe-Kanyiko Wilayani Missenyi na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji
Dr. Iganga Gerrad msemaji wa familia ya Marehemu Bi Esther Rwegasira wakati akitoa neno
Bi Jovitha pichani katikati akijadili jambo wao wanasema 'OKUTEGEKA' na watoto wa Marehemu Tiba na Luta.
Wanaonekana Watoto wa Marehemu Bi Esther Rwegasira katika wimbi kubwa la mawazo, kutoka kushoto pichani ni Luta (Joel),Tiba (Julius) na Joanitha.
Wanaonekana wadau pichani muda
Mdau Kelvin, rafiki wa familia ya Marehemu Bi Esther Rwegasiea
Ikafika fursa ya waombolezaji kupata huduma ya Chakula
Picha ya leo ni Mmoja wa Majah tulioweza kukutana nao katika shughuli ya maziko haya
Huduma safi ya Chakula ikiendelea kwa watu wote waliweza kushiriki shughuli ya maziko hayo
Muonekano wa menu husika.
Kikubwa hapa ni ishu ya mpangilio mzuri wa chakula,hakika jamaa walionekana kujipanga vyema.
Maeneo ya banda ya Mifugo tunakutana na Vijana Ma home Boy wa Kijijini hapa, tunavutiwa na maongezi yao wanavyoendelea 'Kuganyila' na 'Kutensa' kwa namna ya pekee juu ya wema wa Mama huyu Marehemu Ma Esther.
Waombolezaji wakiendelea kupata mulo, hii ni kuanzia saa tano asubuhi mpaka nane mchane kabla ya kuanza kwa Ibada maalum ya maziko ya Mama yetu mpendwa Marehemu Bi Esther Rwagasira
Baadhi ya wanafamilia wakati wa huduma ya chakula
Huduma ya Msosi ikiendelea.
Sehemu ya wanafamilia wakihakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa
Mpangilio mzuri na huduma safi ya Chakula ikiendelea haki bin Sawa kwa watu wote
Muendelezo wa matukio wadau wakiendelea kupata huduma ya Chakula
Nyumbani kwa Marehemu Bi Esther Rwegasira , yalipofanyika maziko yake .
Kufikia hapa BUKOBAWADAU tunakukumbusha kuwa Usisite kutembelea ukurasa wetu wa facebook kwa matukio ya picha zaidi ya 400 na matukio mengine yanayojiri popote pale jiunge nasi kwa ku like' LINK hii BUKOBAWADAU MEDIA
Pichani Bi Esther Rwegasira akitoa sadaka yake kwa mzee Baitromayo Tibawa mkazi wa Kijiji cha Bugombe Kanyigo Wilayani Missenyi,mzee huyu inaaminika kuwa na Umri wa Miaka 105 ,Mzee huyo bado bado ana kumbukumbu ya mengi na yupo imara katiki kufanya shughuli zake kwa kujiongoza mwenyewe.
Naye Mh. Amoody Migeyo Diwani wa Bugandika aliweza kupata fursa ya kutoa Chochote kwa mzee huyo Kikongwe ,Mzee Baitromayo Tibawa mkazi wa Kijiji cha Bugombe Kanyigo mwenye uwezo wa hujiliwaza kwa chupa mbili au tatu za 'Kalinya'
Salaam za rambirambi kutoka kwa Uongozi wa KADEA
Kijana Feruz aliyeweza kushiriki shughuli ya maziko haya
Ni Uzuni na majonzi vikitawala moyoni mwa kila mtu kwa kumpoteza Mama yetu, mlezi wetu, Bibi yet mpendwa Marehemu Bi Esther Rwegasira
Muonekano wa Sehemu ya maegesho
Kupitia Bukobawadau Media tunakufikishia taswira kamili yaliyojiri msibani hapo
Waombolezaji wakiendelea kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Kutoka Mjini Bukoba pichani ni Kijana Martin akiwafariji wafiwa kufuatia msiba huu mkubwa wa Mama yetu mpendwa Marehemu Bi Esther Rwegasira
Mdau Martin akiwafariji wafiwa kufuatia msiba huu mkubwa wa Mama yetu mpendwa Bi Esther Rwegasira
BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 .
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye
Matukio ya picha yaliyojiri msibani hapo
Aliyekuwa mme wa Marehemu Bi Esther , pichani ni Marehemu Balozi Joseph Rwegasira enzi za uhai wake
Bukobawadau tunaendelea kutoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huu pia tunakukumbusha kuwa Usisite kutembelea ukurasa wetu wa facebook kwa matukio ya picha zaidi ya 400 na matukio mengine yanayojiri popote pale jiunge nasi kwa ku like' LINK hii BUKOBAWADAU MEDIA