Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James
Mbatia leo jumanne septemba 13, 2016 wamewatembelea Waathiriwa wa
Tetemeko na kuwafariji Bukoba. Pia waliambatana na Mbunge wa Viti Maalum Bi.Savelina Mwijake na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Chadema.
Mbunge wa Bukoba Mjini akiteta jambo na Wafabiashara mbalimbali walioathiriwa na Tetemeko hilo kubwa Hapa Bukoba na huku kilio chao kikubwa kikiwa ni malimbikizo ya madeni yao kwa serikali ambayo mpaka wanapata hasara kubwa na kwa ujio huu mbaya wa Tetemeko la Ardhi wakidai zaidi ya Milioni 600.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James
Mbatia(kulia) wakimsikiliza kwa makini mfanyabiashara huyo.

Janga la Tetemeko la Ardhi limewaathiri sehemu kubwa wafanyabiashara
Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambae ni Mtaalamu wa Masuala ya Maafa na Mwenyekiti wa Ukawa amewaunga mkono Wanabukoba leo akiambatana na Mwenyekiti mwenza Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe kwenye safari ya kuwatembelea wahanga. Katika Safari hiyo wametoa misaada ya dharura kwa wahanga ikiwemo chakula, sukari, fedha na n.k na kesho Jumatano wataendelea na safari hiyo kuwatembelea Wahanga hapa Mkoani Kagera katika sehemu mbalimbali. Leo wametembelea sehemu ya Kibeta, Hamugembe, Kashozi, Nshambya katika shule ya Ihungo iliyoathiriwa zaidi na Tetemeko hilo kubwa la Ardhi na kuwafanya wanafunzi kusimamisha masomo yao kwa wiki mbili kwa kukosa sehemu ya kusomea/Madarasa na Mabweni.

Msafara kuelekea Kata ya Hamugembe


Pia
walitembelea Kituo cha Watoto Yatima Hamugembe chenye watoto 36 ambacho
kipo chini ya mwangalizi Bi. Saada ambacho kimepata matatizo kwa Nyumba
zake kuanguka chini na kuwapa na kuwafariji

Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe
akisalimiana na Bi. Saada mwangalizi wa Watoto Yatima

Wakiteta na Wanakijiji wa Kibeta sehemu Mama anayotokea Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Muganyizi Lwakatare

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipata Ndizi kwenye Soko la
Nyakanyasi wakati wa kuwatembelea Wahanga wa Tetemeko la Ardhi Bukoba
leo.

Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko

Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini

Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka
Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na
kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya
kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.

Wakiwa Kanisani ndani, Kanisa lililojengwa miaka mingi iliyopita

Akiwa Kanisani hapo alipata muda akafahamu Viongozi mbalimbali katika
picha waliopitia katika kanisa Hilo linalotimiza miaka 125 hivi karibuni
lililozinduliwa mwaka 1892 likiwa ni kanisa la kwanza likifahamika
Kashozi Parish.
Mh. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pia alitembelea Kanisa la Kashozi
Kanisa
la Kashozi kwenye Taswira ambalo pia limepata shida kwenye Tetemeko la
Ardhi lililotokea hivi karibuni siku ya Jumamosi sept. 10, 2016.
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipata nafasi akapata picha na Mama
mlezi kanisani hapo ambaye alitambulishwa kuwa ana umri mrefu