MKOA WA KAGERA WAZINDUA RASMI KAMPENI YA HUDUMA JUMUISHI ZA AFYA NA UKIMWI KATIKA WILAYA ZA MISSENYI NA KARAGWE
Mkoa wa Kagera wazindua rasmi
Kampeni ya Huduma Jumuishi za Afya na UKIMWI yenye Kaulimbiu “Kuwa
Mjanja! Afya ndiyo dili” katika
Halmashauri za Wilaya mbili za Missenyi na Karagwe kwa kulenga kuyafikia
makundi mbalimbali ambayo bado hayaweza kupima afya katika vituo 274 vilivyopo ndani ya mkoa.
Uzinduzi huo wa Kampeni Jumuishi
ya Hudunma za Afya na UKIMWI iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la AMREF HEALTH AFRICA likishirikiana na
wadau wengine ambao ni MDH, HUMULIZA na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera
pamoja na Hospitali za Wilaya za Missenyi na Karagwe ulifanyika katika uwanja
wa Mashujaa Bunazi Wilayani Missenyi.
Akizindua Kampeni hiyo Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu aliwashukuru wadau wote
walioshirikiana kuandaa kampeni hiyo ili kuweza kuwafikia wananchi walio wengi
katika maeneo yao ambao hawajapata wasaa wa kwenda kupima afya zao katika vituo
mbalimbali vya afya mkoani Kagera.
“Uzinduzi wa Kampeni hii
utasaidia wananchi kupima na kujua afya za wale walioathirika na virusi vya
UKIMWI watashauriwa jinsi ya kujitunza na kupewa dawa za kufubaza makali ya
virusi hivyo jambo ambalo litawasaidia wananchi kuyapanga maisha yao mara baada
ya kujua afya zao .” Aliststiza Mkuu wa Mkoa Kijuu.
Mhe. Kijuu aliwashauri wananume
kutoa ushirikianao kwa wake zao pale wanapohitajika kwenda kupima na kuacha
tabioa ya kuamini kuwa wenza wao wakipima tayari na wao wamejua afya zao jambo ambalo siyo sahihi na ukweli ni
kuwa kila mwananchi anatakiwa kujua afya yake yeye mwenyewe.
Akitoa takwimu za Wilaya mbili za
Missenyi na Karagwe Mkuu wa Mkoa Kijuu alisema
kuwa kwa kipindi cha Kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu katika wilaya
ya Missenyi wananchi waliopima ni 57,459 tu wakati Wilaya hiyo inakadiriwa kuwa
na wananchi 202,632 na wananchi 145, 173
bado hawajapima mpaka sasa.
Akitoa takwimu za Wilaya mbili za
Missenyi na Karagwe Mkuu wa Mkoa Kijuu alisema
kuwa kwa kipindi cha Kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu katika wilaya
ya Missenyi wananchi waliopima ni 57,459 tu wakati Wilaya hiyo inakadiriwa kuwa
na wananchi 202,632 na wananchi 145, 173
bado hawajapima mpaka sasa.
Katika Wilaya ya Karagwe wananchi
waliopima ni 50,797 kwa kipindi cha Januari hadi Julai 2016 na Wilaya hiyo
inakadiriwa kuwa wananchi 332, 020 ambapo wanachi 281,223 hawajapima kujua afya
zao katika Wilaya hiyo jambo ambalo sasa wamepata fursa ya kupima afya zao bure
bila malipo yoyote.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.
Thomas Rutachunzibwa alisema kuwa lengo la Kampeni hiyo ni kutoa huduma ya
upimaji bure kwa wananchi ili makundi mbalimbali yaweze kufikiwa kwa muda mfupi
na kuwahamsisha wananchi kupima kwani walio wengi wanaogopa kupima kwasababu ya
gharama za upimaji.
Aidha Dk. Thomas alisema lengo lingine
ni kuhakikisha kuwa asilimia 90% ya wananchi katika Wilaya hizo wanapima,
wagonjwa ambao wakigundulika kuwa tayari wameathirika asilimia 90% wapate dawa za kufubaza makaili
ya virusi vya UKIMWI pia na kupewa huduma za ushauri nasaha.
Wanaonekana wanafunzi pichani
Katika Halmashauri za Wilaya
mbili za Missenyi na Karagwe Kampeni ya huduma Jumuishi za Afya na UKIMWI
itafanyika kakika kata 10 kila Halmashauri kwa siku mbili ambapo kwa Missenyi
kata hizo ni Buyango, Bwanjai, Kanyigo, Kyaka, Gera, Ishozi, Kashenye, Kasambya,
Mutukula na Minziro.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya
Karagwe Kampeni hiyo itafanyika katika kata za Kihanga, Kanoni, Kayanga,
Bugene, Nyakabanga, Nyaishozi, Kamagambo, Kibondo na Nyakasimbi. “Kuwa
Mjanja! Afya ndiyo dili”
Katika picha ya pamoja
Na Sylvester Raphael