Mkoa wa Shinyanga watoa zaidi ya milioni 41kusaidia waathirika wa tetemeko Kagera
Mkoa wa Shinyanga
umekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya Sh. milioni
41,172 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ili kusaidia waathirika wa tetemeko la
ardhi lililotokea mkaoani humo hivi karibuni.
Makabidhiano hayo
yalifanywa leo mjini Bukoba kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu
Telack ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa na viongozi wa dini
ambapo mkoa wa Kagera umewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali
Mstaafu Salim Kijuu.
Wananchi wa mkoa wa
Shinyanga wameguswa na kadhia iliyopata wananchi wa Kagera, hivyo tukaamua
kukusanya nguvu ya pamoja kama mkoa ili kuwafariji Watanzania wenzetu kutokana
na matatizo waliyoyapata” alisema Bi Zainabu.
Mkuu huyo wa mkoa
alifafanua mchango wa misaada waliyotoa kuwa ni paamoja na mabati ya geji 28
1400, saruji mifuko 750, mchele kilo 600, mahindi kilo 100 paamoja na nguo.
Bi.Zainabu aliongeza
kuwa michango ya msaada huo imeunganishwa nguvu kutoka Serikali ya mkoa wa
Shinyanga, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, sekta binafsi,
masshirika ya dini, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mogodi ya madini iliyopo
mkoani humo na wadau wengine wa maendeleo.
Akitoa shukrani mara
baada ya kupokea msaaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa
kuwafariji, majitoleo yao kwana kuwajali katika kipindi hiki cha mpito cha
athari za tetemeko lililoukumba mkoa huo.
Na Eleuteri Mangi,
MAELEZO, Bukoba