Mkurugenzi wa World Share Kim, Na Ra atoa taa za sola 70 ili kuwasaidia waathirika wa Tetemeko kagera.
WAATHIRIKA
wa tetemeko la Ardhi wanaoishi katika maeneo ya Bilongo kata Minziro
kijiji kigazi wameilalamikia serikali kutokana na msaada mdogo
unaotolewa kwao kutokidhi mahitaji yao kulingana na walivyothirika.
Malalamiko
hayo yametolewa kutokana kupatiwa vyakula kidogo na wakati mahitaji
yao yakiwa ni mkubwa kwakuwa athari waliyoipata imewapelekea kuharibu
kila kitu chao na kusababisha kukosa chakula hadi sasa.
Hayo
yalibainishwa na baadhi ya wananchi waliopoteza makazi yao wakati wa
tetemeko ambao Yasinta Patrick na Agnes Sedhalio walibainisha hayo
wakati walipotemberewa na mkurugenzi wa (World Share) Shirika
linalojishughusha na watoto yatima na alibino Kim,Na Ra raia wa kolea
kusini ambae pia alitoa taa za sola 70 kwaajili ya waathika hao ili
ziweze kuwasaidia nyakati za usiku wanapokuwa katika mahema yao ambayo
ni makazi yao muda.
Hata
hivyo Yasinta Patrick mama mwenye watoto saba alisema kuwa serikali
ilipo pereka misaada ili waperekea mchere kilomoja na nusu, unga
kilomoja na Nusu Maharagwe kilo mbili, na Sukari nusukilo, pamoja na
bisukuti pakiti tano.
Patrick
alisema kuwa chakula hicho wanacho pewa na serikali hakitoshi katika
familia ya watoto saba maana kwa sasa hawana makazi zaidi wanautumia
muda mwingi kulinda mali zao.
"Jamani
Serikali itufikilie maana chakula hicho tunachopewa hakitoshi hata siku
mbili kwa familia kama yangu mimi mwenye watoto wengi na mimi
pia"alisema Patrick
Agnes
Sedhalio alisema kuwa serikali iwatumie watu wanaoaminika katika kugawa
misaada hiyo kwa jamii maana wanapo kuja kutugawia hiyo misaada hata
hawatuthamini kama sisi ni watu kama watu wengine.
"Hivi
unga kilomoja na nusu na mchere kilomoja na nusu kweli unatosha au
nikutudhihaki' mfano mimi wananiletea bistukut ili niwape watoto wale
kweli au maji chupa moja ni kwanini wasitulete chakula moja kwa moja
tukajua moja kwakweli inasikitisha sana kwa mambo tunayofanyiwa"alisema
Sedhalio
Naye
mwenyekiti mstafu Godfry Kagoro alisema kuwa katika kijiji cha Kampaini
kilichopo mpakani mwa Tanzania na Uganda alisema kuwa katika eneo hilo
kuna zaidi ya wananchi 200 lakini waliopewa mahema na hivyo vyakula
kidogo ni familia saba tu wanaoishi barabarani tu.
Kagoro
alisema kuwa tetemeko hilo baada ya kupita limeharibu utalatibu wa
maisha ya kawaida hivyo kuna hatali ya watu kufa na njaa.
"
Kwa sasa hatuna chochote kile zaidi ya kuanza ujenzi wa nyumba kwa
upya na hatujui hatima ya serikali kwa familia zetu waliokuwa wanakweda
kuhangaika kutafuta riziki sasa hawaendi, wakati mwingine tunaogoka
kwamba tukitoka litajirudia tena jamani serikali itupe msimamo kamili
juu ya tetemeko hili"alisema Kagoro
Pia
wananchi hao wametoa ombi lao kwa mbunge wa jimbo la Nkenge Dr Diodorus
Kamala kuludi jimboni ili aweze kuwasaidia katika kuwabaini waathilika
kiundani maana walio wengi hawaja fikiwa na watoa tathimini.
Mwisho.