Bukobawadau

SIKU YA UTALII DUNIANI 27 SEPTEMBER 2016 NA CHANGAMOTO ZA TETEMEKO MKOANI KAGERA

Siku ya Utalii Duniani husherehekewa na nchi za Umoja wa mataifa kila mwaka tarehe 27 September. Mwaka hu inakumbukwa hapa mji wa Bukoba tukiwa kwenye maafa ya tetemeko la ardhi. Watu mbali mbali mbali kutoka pande zote za dunia wanasikia juu ya mji wetu na wengi wamesafiri na wengine bado wanapanga safari kuja hapa kutuona, kutufariji na vilevile kutusaidia kupunguza makali ya janga la tetemeko lililoukuta mkoa wetu wa Kagera. Kwa maneno mengine utalii wa namna hii unaitwa utalii mweusi. Yaani utalii unaotokana na maafa kama vita, mafuriko, matetemeko na kadhalika.
Sisi wadau wa utalii tunatoa pongezi kuubwa sana kwa vyombo vya mawasiliano simu na mitandao ya internet pia watoa habari woote. Usambaji wa habari ni muhimu katika kumfanya mtu apange na kuondoka mahali pake anapoishi na kuchukua usafiri kwenda anapotarajia kufika.
Pili pongezi kuubwa kwa vyombo vya usafirishaji Ndege zetu za Auric Air, Precision Air na wasafirishaji wa barabara ambao woote wamefanikisha kuwafikisha wageni wetu hapa Bukoba na maeneo halisi kwa ufanisi wa hali ya juu. Ni masikitiko kuwa usafiri wa majini hadi sasa haupo na wengi wangelipenda kutumia usafiri huo.
Pongezi pia ziende kwa vyombo vya usalama kama polisi, kamati ya usalama ya mkoa, walinzi na jeshi ambao katika hali ya taharuki iliyofutia tetemeko wamechangia sana wageni wetu kukuta mahali hapa panafikika na utendaji wa kilichowaleta unaenda bila wasiwasi.
Pongezi za zaidi ziende kwa sehemu zoote za kulala wageni na huduma za chakula. Ama kweli mahoteli ya hapa mjini Bukoba na guest kama zisingekuwapo na kufanya kazi nzuri wageni wote hawa wangepata adha kubwa.
 Athari ya Tetemeko, hapa ni shule ya Sekondari ya Nyakato
 Matukio mbalimbali ya Utalii Mkoani Kagera
Mwaka huu siku ya Utalii duniani hapa Kagera inakuta mambo kadhaa yanayoelekea utalii

1. Makumbisho Majengo ya zaidi ya miaka mia yameanguka au kuharibiwa na tetemeko la aridhi. Haya ni kama
i) Kanazi Palace and Museum iliyoko Kanazi Bukoba vijijini
ii) Kanisa la Kashozi (Kanisa la kwanza wakati mapadre wafaransa wa White fathers wanaingia Bukoba kuingiza dini kutoka Uganda
iii) Kanisa na shule kongwa ya Ihungo secondary school
iv) Misikiti ya zamani
2. Sikukuu ya miaka mia kuanza kwa mapadre hapa Kagera huko Rubya. Wanategemewa wageni wengi kutoka nchi mbali mbali za Tanzania

3. Hija kuubwa ya kila mwaka ya Nyakijooga mwezi wa October

Makadirio ya watalii wanaoingia Bukoba kwa wakati huu ni 750 kwa mwaka wengi kabisa wanatoka Ujerumani na kufuatiwa na nchi nyingine za Uropa kisha marekani pia.
Changamoto zilizopo hadi sasa ni jinsi ya kuongeza ubora wa huduma kwenye mahoteli, sehemu za chakula na kwenye vivutio vya utalii. Tunahitaji pia kuongeza ubora wa hoteli kueleka viwango vya kimataifa
Mwisho Pendekezo kubwa ni Mkoa kushirikiana na wadau wa utalii kutengeneza Makumbusho kubwa ya maafa mbali mbali ambayo yamekuwa yakiukumba mkoa wetu. Taarifa zitakazokuwa humu kwenye makumbusho zitasaidia kukabiri majanga mengine yakijitokeza miaka ya mbeleni.
 Utalii ni nguzo kubwa ya uchumi wetu. Watalii hutuingizia fedha tena za kigeni na pia hutengeneza ajira mbali mbali na kipato kwa watu wengi wanaouuza na kutoa huduma mbali mbalimbali.

Ingawa utalii ni biashara, Utalii unatofauti na biashara nyingine kama kuuza sementi au mabox ya dawa za meno, kwa maana sio hesabu tu ya watalii wangapi wameingiza pesa ngapi. Utalii kwa namna nyingine kwa kihaya tunasema
"OBUKWATANE KAGURU"
Hii inamaanisha kuwa kwa kutembeleana inaleta urafiki, inaleta faraja, kujifunza juu ya wenzako na mila na desturi zao na pia kujenga maelewano mazuri.
Next Post Previous Post
Bukobawadau