Bukobawadau

#TETEMEKOBUKOBA :WATU 10 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA


Mjini Bukoba hali ya taharuki imewakumba wakazi wa Mji huobaada ya kutokea tetemeko la ardhi lililodumu kwa takribani dakika tatu na kusababisha nyimba kadhaa kubomoka, Vifo, Majeruhi na majengo ya hoteli na nyumba za makazi kukimbiwa,pichani ni muonekano wa baadhi ya majengo katikati ya Mji wa Bukoba yakiwa yamebomoka #TetemekoBukoba
Madhara makubwa yamejitokeza na kusababisha Nyumba nyingi kubomoka hasa maeneo ya Kashura na Hamugembe ndani ya manispaa ya Bukoba,taarifa rasmi zinasema tayari Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbaz Msuya yupo njiani kuelekea Bukobana kufikia kesho saa tano waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa atakuwa amewasili mjini hapa #Tetemeko bukoba

Watu 10 Wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jioni ya leo Mjini Bukoba na maeneo ya Jirani #TetemekoBukoba
Hali ya Majeruhi hospitali wakipata huduma
Baadhi ya Majeruhi wa tetemeko la ardhi wakipata msaada wa huduma ya kwanza katika hospitali ya mkoa Kagera.#TetemekoBukoba

Muendelezo wa matukio kutoka hospital ya Mkoa Kagera
Majeruhi wakiendelea kupata huduma ya kwanza
Mashuhuda wa tukio
Hali yasintofahamu kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakiwa wamekusanyika nje ya lango la Hospitali kuu ya Mkoa Kagera


Hali ya barabara ya Kasarani kuelekea Custam (Uganda road)#TetemekoBukoba
RPC Kagera Augustine Ollomi amethibitisha idadi ya Vifo na majeruhi waliojitokeza #TetemekoBukoba


Jengo la Mukhpar wauzaji wa pembe jeo za Kilimo mjini Bukoba likiwa katika hali hii...
#TetemekoBukoba
Jengo la Ofisi ya Bwana Jamal Kalumuna likiwa limekumbwa na tetemeko hilo lililotokea jioni ya leo Mjini Bukoba
Jengo la Haji Abdulziad Kashinde likiwa limeharibika vibaya




Nyumba mbalimbali za makazi zikiwa zimekumbwa na tetemeko,hapa ni maeneo ya Kashura.

Maeneo ya Kilimahewa-Kashai Bukoba


Binti Ziadi Pichani akipata huduma katika hospital ya Mkoa, kwa ufupi ni kwamba hali ni mbali kuliko unavyo weza kuchukulia kwa haraka...
Buruhani Kichwabuta akiwa hoi kufuatia majeraha aliyoyapata.

Majeruhi wakiendelea kupata huduma
Bukobawaau tunatoa pole kwa wana Bukoba kwa hali ya taharuki iliyojitokeza kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea muda wa Saa 9:30 alasiri Sep 10, 2016,Kwa ufupi athari kubwa imejitokeza ...kama inavyo onekana kupitia picha, Nyumba nyingi zimebomoka na nyinginezo kupata nyufa
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ihungo wakisubili huduma katika hospitali ya Mkoa Kagera#TetemekoBukobaIdadi kubwa ya Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya matibabu ,tunaenelea kusubili taarifa zaidi na ufafanuzi kutoka katika mamlaka husika.

Jengo la fidodido

Barabara zikiwa zimekubwa na mtikisiko Manispaa Bukoka #MajangaKagera #TetemekoBukoba

Picha zote na Bukobawadau Blog

Earthquake measuring 5.7 hits northwest Tanzania - USGS
An earthquake measuring 5.7 hit northwest Tanzania on Saturday, 44 km from Bukoba, close to the western shore of Lake Victoria, the U.S. Geological Survey reported.
The quake, recorded at a depth of 10 km, struck at 12.27 p.m. GMT (5.57 p.m. IST), the report added.
Atleast 10 people have been killed and More than 100 reported injured in the quake, which hit Kagera region on the western shore of Lake Victoria, regional police commander Augustine Ollomi said.
Widespread damage was reported following the quake, which also rocked the neighbouring regions of Mwanza, Mara and Simiyu.
The quake had its epicentre in Tanzania, according to sources at a volcanic observatory in the Congolese city of Goma, where the quake was also felt.
Next Post Previous Post
Bukobawadau