TTCL na TPDC zatoa milioni 30 kusaidia waathirika tetemeko Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salim Kijuu (kulia) akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600
ya saruji ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akipokea msaada uliotolewa na Bodi ya TPDC (kushoto).
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses msaada ambao unalenga
kuwasaidia kurekebisha makazi ya waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa
huo.
Picha na Eleuteri
Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Wafanyakazi na
Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wametoa msaada wa
Sh. milioni 20 kusaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa waathirika wa tetemekola
ardhi mkoani Kagera.
Akikabidhi msaada huo
kwa Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu, Mwenyekiti wa Bodi
ya TPDC Balozi Dkt. Ben Moses amefafanua kuwa msaada huo unalenga kuwasaidia
kununua mabati na saruji kwa waathirika wa tetemeko hilo lililoukumba mkoa huo.
“Sisi TPDC tunatoa
msaada wetu kama sehemu ya Watanzania na tatizo hili ni letu sote na Watanzania
ni wamoja” alisema Dkt. Moses.
Kwa upande wake Meja
Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru TPDC kwa mchango wao na kubainisha kuwa
hakuna kitu kidogo katika kutoa na kuwahakikishia wadau wote wanaotoa michango
yao kuwa misaada hyote inayotolewa itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na itasaidia
kuwarudishia makazi waathirika wa tetemeko hilo.
Aidha, Mkuu huyo wa
mkoa amewataka watu wote wenye mapenzi mema kuendelee kuwachangia waathirika wa
tetemeko hilo na waige mifano ya watu na taasisi mbalimbali wanaoendelea kutoa
misaada kwa mkoa wa Kagera ili kuwarudishia makazi wananchi walioathirika maafa
hayo.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa TPDC Kapuulya Musomba
amesema kuwa huo sio mwisho wao katika kuchangia waathirika wa tetemeko
la ardhi, bali wanaendelea kuwahamasisha wadau wa mafuta na gesi yakiwemo
makampuni ya ndani na nje ya nchi ili kuwafanya wananchi waweze kuendelea na
kazi zao za kila siku kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) nao wametoa msaada wa mifuko saruji 600 ambayo
ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10 ikiwa ni mchango wa wa
kampuni hiyo katika kuwashika mkono na kuwafuta machozi wananchi wa Kagera.