WAHUKUMIWA MAISHA KWA UCHOMAJI WA MAKANISA MKOANI KAGERA
Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba imewatia hatiani na kuwahukumu kwenda
jera kutumia kifungo cha maisha watu watatu ambao ni pamoja na Ngesella
Joseph, Rashid Mzee na Ali Dauda waliokuwa na tuhuma ya kuhusika na
vitendo vilivyokuwa vimekithiri mkoani Kagera mwaka jana vya uchomaji wa
makanisa ya madhehebu ya kikristo katika maeneo mbali ya mkoa huo.