Bukobawadau

WAJASIRIAMALI BUKOBA WATOA YAMOYONI

Wajasiriamali wa soko kuu mjini Bukoba mkoani Kagera wameeleza jinsi uchumi wa biashara hiyo ulivyo yumba kutokana na Tetemeko la ardhi lililopita septemba 10 mwaka huu .
Na Renatha Kipaka
Bukoba.

Kauli hizo zimetolewa na baadhi ya wafanyabisha wa samaki , Nyama, pamopa na nafaka nakusema kuwa toka tetemeko lipite mpaka sasa hawapati wateja kabisa kiasi kwamba kuna wakati mwingine bidhaa zao hazitoki kabisa.
Wafanyabiashara hao ni Revina Erenesti na mkazi wa Hamugembe Kashabo,Tirifina Chalesi mkazi wa Buyekera Gengeni, Serina Godwini mkazi wa kata kashai mtaa wa Kilimanjaro, wote hao wachuuzi wa samaki wakavu katika soko kuu la Bukoba Manispaa.

Erenesti alisema kuwa toka tetemeko lipite biashara ya samaki imekuwa ni kitendawili kwani mauzo aliyokuwa akiyapata hapo awali kabla ya janga hilo alikuwa akiiuza zaidi ya shilingi 30000 hadi 50000.

“Mimi ni mama wa familia lakini toka tetemeko limetokea tunaishi kwa shida sana na watoto biashara haindi wakati huo watoto wanahitaji mahitaji ya kila siku tunalala nje jamani serikali itukumbuke kutupa chakula pasipokuwa na makazi ya kuishi ni shida sana watoto wanag’antwa na mbu ikiwa viongozi wa mkoa wasliahidi kuleta neti hazifiki kwa kweli inasikitisha sana”alisema Erenest

Tirifina Charles alisema mchuuzi wa samaki wakavu alisema kuwa sasa anashinda amekaa hauzi anashinda na mzigo wa samaki mpaka jioni bila kuuza hata shilingi mia moja kitu ambacho kimekuwa hatali kwa maisha yao.


“Mimi kwakweli hali yangu imekuwa ngumu zaidi, serikali itusaidie kutujengea hata chumba kimoja na sebule ili niweze kukaa na watoto jamani kutupa vyakula bila sehemu ya kulala tuna teseka sana”alisema Charles


Serina Godwini alisema kuwa kwasasa amepata ugonjwa wa kifua kiasi kwamba anauza samaki akiwa amelala kwenye meza anayofanyia biashara yake.

“Naiomba serikali inisaidie angalau inijengee hema hata moja tu niweze kulala na watoto wangu maana kadri barilidi inavyooenderea kutuingia hapo baadae inaweza kuniletea shida kiafya kwangu na kwa watoto wangu ambopo itasababisha kutumia garama kubwa za matibabu tubu madhara hayo”alisema Godwini

 Nao wauza nyama katika soko hilo wametoa changamoto walizokumbana nazo kwenye biashara zao zimesimama kiasi cha kutoka kuuza kilo 150 za nyama mpaka kufikia kilo 30 kwa siku.

Wauza nyama Hamza Venanti alisema kuwa toka tetemeko limetokea biashara hiyo imekuwa ngumu japo kuwa bei haijapungua lakini wateja hawapo .


“Mimi familia inanitegemea wakati huo nyumba yangu imeanguka sijui nitaanzia wapi mpaka muda huu, serikali inisaidie ili niweze kupa angarau bati, nondo, simenti na pesa ili tuweze kujenga upya makazi maana tuna hangaika sana”alisema Venant


Abually Said mfanyabiasha wa bucha ya Nyama mkazi wa Kashai Matopeni alisema tetemeko hilo lilipotokee familia yake imeongezeka kwani anaishina ndugu zake waliobomokewa nyumba zaona kwenda kuishi kwake mpaka watakapo pata makazi yao.


“Yaani Serikali iwasaidie waathirika mapema maana mimi nilikuwa na nishi na mke wangu pamoja na mtoto wetu wa miwezi mine sasa wameongezeka ndugu zangu sita na kipato changu ni kidogo jamani wakumbukwe halaka ili nipate pumzi”aliseama Said

Naye Alphan Amada mfanyabiashara wa nyama na mkazi Kashenye Kashai alisema kuwa mtu anapo pewa simenti 5 , na mabati 20, ni bora watu wapewe mitaji maana watakapo wapa watu vitu hivyo na wakati hawana chochote hawatajenga maana hawana pesa za kuwalipa mafundi.
“Mimi binafisi naishauri serikali iwape watu pesa maana hali ni ngumu sana vinginevyo watu wataopewa hivyo vifaa wataishia kutumia tu hizo pesa na kuenderea kunyeshewa na mvua pasipo kujenga maana watu ni watupu”alisema Amada
Halima Issaka muuzaji wa nafaka alisema kuwa biashara hiyo imekuwa ngumu kwakuwa kwasasa anauza shilingi elfu 3000 tu tofauti na hapo mwanzo alipokuwa akiuza zaidi ya shilingi elfu 50000 kwa siku.

“Mtu unakuja sokoni una panga mchele, maharagwe, pamoja na ulezi patupu hata pesa ya kula inakosekana kwa siku ‘mfano mimi kwangu huwa ninatumia shilingi elfu 7000 sasa hata hiyo siipati hivi nitishia wapi mimi”alisema Issaka
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau