WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO KUJIONEA ATHARI ZA TETEMEKO LA ARTHI
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa atembelea Shule ya shule ya sekondari ya
Ihungo kujionea athari iliyojitokeza kutokana na tetemeko la ardhi
lililotokea jana tarehe 10/09/2016 katika Mkoa wa Kagera na baadhi ya
maeneo ya Mkoa wa Mwanza na Shinyanga.#TetemekoBukoba.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa
alisema tayari ofisi yake imetuma Wataalamu wa kitengo cha maafa ili kufika Mkoani
Kagera kufanya tathimini ya kina na ya haraka wakishirikiana na kamati ya maafa
ya mkoa ili kubaini ni sehemu gani zinazohitaji huduma au msaada wa haraka ambapo
janga la tetemeko limesababisha madhara makubwa.#TetemekoBukobaWaziri Mkuu Kassimu Majaliwa alisema tayari ofisi yake imetuma Wataalamu wa kitengo cha maafa ili kufika Mkoani Kagera kufanya tathimini ya kina na ya haraka wakishirikiana na kamati ya maafa ya mkoa ili kubaini ni sehemu gani zinazohitaji huduma au msaada wa haraka ambapo janga la tetemeko limesababisha madhara makubwa.
Jengo la Kanisa la Shule ya Sekondari Ihungo likiwa limebomoka kutokana na tetemeko la ardhi
lililotokea jana tarehe 10/09/2016
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiendelea kukagua maeneo ya Shule ya Sekondari IhungoMuonekano wa Ndani wa Kanisa la Shule ya Sekondari ya Ihungo
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasiili Mkoani Kagera majira ya saa 7:00 mchana aliwatembelea majeruhi waliojeruhiwa wakati wa tetemeko hilo ambao bado wamelazwa katika Haspitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, pia alitembelea shule za Sekondari za Nyakato na Ihungo ambako madhara yalitokea makubwa na kupelekea wanafunzi kukosa sehemu za kulala baada ya mabweni yao kubomolewa na tetemeko.
Vile vile Mhe Majaliwa alishuhudia maiti 14 na kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu katika uwanja wa Kaitaba ambapo marehemu hao waliombewa dua na sala kutoka kwa viongozi wa dini Mkoani Kagera . Pia Mhe. Majaliwa aliwapa pole wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokusanyika uwanjani hapo kwa kuwapa salaam za Serikali.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ihungo
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa (katikati) akitoa pole kwa Walimu na Wanafunzi wa Shule ya shule ya sekondari ya Ihungo wakati akipotembelea shule hiyo mapema ya leo Sep 11, kujionea athari iliyojitokeza shuleni hapo
Waziri Mkuu akisalimiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ihungo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiendelea kukagua athari iliyojitokeza katika shule ya Sekondari ya Ihungo
Hali ilivyo katika shule ya Shule ya Sekondari ya Nyakato #TetemekoBukoba