Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aipongeza Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa namna ilivyokabiliana na Athari za Tetemeko
#TetemekoBukoba Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa aipongeza Serikali ya mkoa wa Kagera kwa namna ilivyokabiliana na athari za tetemeko
Aahidi mifuko 400 ya cement itakayokabidhiwa kesho kwa ajili ya
kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi,aonyesha kukerwa na mabomu.
Kauli hiyo ilitolewa na Lowassa wakati alipoingia katika ukumbi wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salimu Kijuu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa siasa pamoja na kiongozi wa dini.
Kauli hiyo ilitolewa na Lowassa wakati alipoingia katika ukumbi wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salimu Kijuu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa siasa pamoja na kiongozi wa dini.
Viongozi
hao ni aliekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,
Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini,Alhaji Rajabu kutoka katika jumuiya
ya kisilamu.
Hata hivyo alisema kuwa Simenti
hiyo itakabidhiwa lasimi kesho mapema na Meya wa Manispaa ya Bukoba Chifu
Kalumna ili kuendeleza kuwasaidia
waathirika wa tetemeko la ardhi waliopoteza makazi.
Aidha
Lowassa amesema kuwa kuna kila sababu ya serikali kupitia kamati ya
maafa kuandaa vipindi maalum kupitia runinga ili kuwafamisha watanzania
ukubwa wa tatizo liliopo mkoani Kagera
Pia Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Msitaafu Salimu Kijuu ametoa shukrani
zake kwa viongozi hao kwa msaada mkubwa wa simenti mifuko 400.
Katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Msitaafu Salimu Kijuu
Credit:Renatha Kipaka,Bukoba.