Bukobawadau

YANAYOJIRI KATIKA KUCHANGIA WAHANGA #TETEMEKOBUKOBA

Shukrani kwako Mh.KNape Moses Nnauye asante kwa jitihada hii. Bukobawadau tunashauri tupate nakala ya Kiingereza pia maana ukubwa wa janga la #TetemekoBukoba ulieleweka na kugusa mioyo ya watu wa nje mapema zaidi kuliko vyombo na mashirika ya ndani. Tatizo lililokuwepo kiasi kwamba watu binafsi wa nje ya nchi kushindwa kuchangia ni ukosefu wa Taasisi inayoaminika. Sasa utaratibu umewekwa itakuwa vizuri wafahamishwe.
#TetemekoBukoba

#TetemekoBukoba;Wafanyabiashara/Mabalozi waahidi na kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi Bukoba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azungumza na wadau kuwaomba kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Bukoba.
Waziri Mkuu anatoa hali halisi ya namna maafa yalivyo athiri maeneo ya Bukoba.
Waziri Mkuu anasema wadau wanaweza kuchangia kupitia njia mbalimbai zikiwemo njia za Mitandao ya simu.
Waziri Mkuu anatuma salamu za shukrani kutoka kwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
========
ORODHA YA MICHANGO KUTOKA KWA WADAU NA MABALOZI:

= Balozi wa Zimbabwe (Ambaye ni kiongozi wa Mabalozi) sasa amealikwa kuzungumza kwa niaba ya Mabalozi woote walioko nchini, anaanza kwa kuonyesha masikitiko yake juu ya janga hili lililoikumba Tanzania.
= Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi sasa amealikwa kuzungumza kwa niaba ya wadau wa sekta binafsi nchini.
Anaanza kwa kuihakikishia serikali kuwa wako nyuma ya Serikali katika hili na anaona ni vizuri kuipongeza serikali kwa hatua za awali ilizochukua lakini misaada ya kwanza na ya nguvu itatoka kwao wafanyabiashara wa Tanzania.
Reginald Mengi anasisitiza kuwa wafanyabishara wanaihakikishia serikali kuwa watatoa michango ya hali na mali.
= Watumishi wa Wizara ya Mambo Ya Nje wachangia milioni 10 kwa ofisi ya Waziri Mkuu.
= Jumuiya ya raia wa China wapewa nafasi ya kuzungumzia na muwakilishi anaanza kuelezea kwanini jamii ya wachina imeguswa na majanga na kuchangia Milioni 100 za Kitanzania.
= Muwakilishi wa UN sasa amealikwa kuzungumza katika halambee hiyo anasema wanatapenda kujua kila tathmini inayofanyika katika eneo la Bukoba lakini wanasikitika kuwa wanamawakala wa UN wachache kwa hapa Tanzania.
Anataja maeneo ambayo yatahitaji msaada na anaahidi kuwa siku ya jumamosi watatoa msaada wao wa hali na mali.
= Ubalozi wa Kuwait wanatoa michango yao ya fedha kwa viwango mbalimbali Euro, Tsh na Doller
= Balozi wa Kenya sasa amealikwa kuzungumza na kwa kuanza anawakilisha majonzi ya Wakenya na anaongeza kuwa katika hali kama hii kuna mambo mengi yanahitajika kusaidiwa ikiwemo malazi, anasema wao kama Wakenya watatoa zaidi ya michango waliyokwisha itoa hivyo wataongeza Mablanket, Vifaa vya Ujenzi, na Afya.
= Wadau kutoka China tena wanaongeza kiasi cha Milioni 100 kuchangia waathirika wa tetemeko Bukoba na viunga vya jirani.
= Balozi wa Japan nchini Tanzania anaanza kwa kutoa historia ya urafiki wa Tanzania na Japan na kutoa pole zake za dhati.
= Mohamed Dewj Enterprises anachangia Milioni 100 kwa wahanga wa tetemeko.
= Balozi wa Korea Kusini wanaahidi kutoa misaada ya kibiaadam na anatoa pole za dhati kabisa.
= Muwakilishi kutoka sekta ya Mafuta (Wafanyabiashara wa Mafuta) wanaomba muda na kesho watatoa msaada wao kwakuwa wengi wa wadau hawapo.
= TBL Wamechangia Milioni 100
= Azania Group Wanatanguliza Milioni 20
= Wafanyabiashara wa Mafuta wa rejareja watakusanya Milioni 250 na watakabidhi ijumaa ya week hii
= Kagera Sugar wanatoa Milioni 100 na tani 10 za sukari.
= Serengeti wanatoa saruji mifuko 800
= Pepsi Cola 50 Millioni
= Hatiamaye Regnald Mengi anatoa mchango wake wa Milioni 110.
= Protas Ishengoma anatoa msaada wa Milioni 5.
= GBP, MOIL na OILCOM wameahidi kujenga shule mbili (Ihungo na Nyakato) zilizoharibiwa vibaya.
= Puma wanachangia 50 Milioni
= Agusta Tanzania wanatoa Milioni 10
= Camel Oil wanachangia mifuko 1,000 ya Cement
= Tippa waachangia milioni 20
= Orexy wanachangia Milioni 50
= Waislamu wa madhehebu ya Al-Shafy, Ijumaa na Adhuhuri wanachangia Milioni 1.
= Sahara Tanzania wanachangia Milioni 20
Wizara ya Mambo ya Nje watafanya matembezi ili kuhamashisha uchangishaji wa fedha na wataanzia Polisi Oysterbay.
MAJUMUISHO:
Waziri Charles Mwijage nafanya majumuisho ya fedha zilizopatikana ni kama ifuatavyo:
1. Fedha taslimu ni Milioni 646,
2. Ahadi ni Milioni 705,
3. Dola za Kimarekani 10,000
4. Yuro 10,000.
5. Mfuko ya Sementi zaidi ya 2800,
6. Ahadi ya ujenzi wa Shule mbili ndani ya siku 30.
JUMLA KUU, Bilioni 1 na Na Zaidi ya Milioni 300
======

Ahsanteni kwa kuwa nami........
Next Post Previous Post
Bukobawadau