Bukobawadau

BALOZI DR KAMALA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KIJIJI CHA KYAZI - KITOBO

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala leo Oct 6,2016 ameendelea na ziara yake Jimboni , ziara yenye lengo la kuwapa pole wananchi kwa Tetemeko la ardhi lenye uzito wa 5.7 katika vipimo vya richa lililotokea eneo la Kaskazini Magharibi mwa Tanzania karibu na ziwa Victoria na asa mkoa wa Kagera pamoja na Jimbo la Nkenge
 Katika Mkutano huo  pia, Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za za wananchi  na kufuatia Taarifa ya Kijiji na Kata inaonyesha wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha na baadhi ya maeneo Umeme haujafika. Kamala ameahidi kushughulia kwa haraka kero hizo pamoja na tatizo la maji walilonalo wananchi wa Vijiji Kyazi,Mbale na Kashasha .
Aidha Balozi Dr.Kamala amesema hatua za haraka zinatakiwa kukabilina na hali ngumu ya kiuchumi inayotokana na athari ya Tetemeko ,Ukame na Kiangazi.
 Muonekano wa Ngoma ya Kijiji inayotumika pala linapotokea jambo lolote linalohusiana na wananchi
 Pichani anaonekana Bw.Boniface B.Rweyemamu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyazi-Kitobo akisoma taarifa fupi ya serikali ya Kijiji hicho kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala katika ziara yake ya kutoa pole na kupokea kero mbalimbali.
 Bi Hilda pichani katikati ambaye ni Kiongozi wa Kikundi cha akinamama cha 'Abagambakamo' akisoma Risala ya kikundi chao kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa
 Vikundi vya Wanawake vya Wajasiriamali vya kujikwamua kiuchumi ''Abengozi Kyazi'wakitoa zawadi kwa
Mbunge wa Nkenge Balozi Dr Kamala

 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mgombea Mbunge wa Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya akinamama  wa Kijiji Kyazi kata Kitobo
  Mwenyekiti wa Kikundi cha akinamama cha 'Abagambakamo' Kyazi Bi Hilda akikabidhi Risala yao kwa Mbunge wa Nkenge Balozi Dr Kamala
 Baadhi ya akinamama hao wakisalimiana na Diwani wa Kitobo Mh.Willy Mtayoba
Kushoto ni Bw. Mdhahiri Dreva wa Mbunge Balozi Dr. Kamala na Kulia ni Katiwa wa Mbunge  Bw. Joansen Kato wakiwa na zawadi alizo kabidhiwa Mbunge kutoka kwa akina mama wa Vikundi vya 'Abengozi' na 'Abagambakamo' wa Kyazi Kitobo Wilani Missenyi
 Diwani wa Kitobo Mh.Willy Mtayoba katika Mkutano wa Mbunge Nkenge Balozi Dr Kamala uliofanyika katika Kijiji cha Kyazi Kitobo Oct 6,2016
 Mbunge wa Nkenge, Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala  akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kitogoji cha Kyazi juu ya changamoto pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo yeye na Rais Magufuli, pamoja kuangalia maendeleo katika Kijiji hicho, Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala amewapa pole kwa Tetemeko la ardhi lenye uzito wa 5.7 katika vipimo vya richa lilitokea tarehe 10 Sep eneo la Kaskazini Magharibi mwa Tanzania karibu na ziwa Victoria na asa mkoa wa Kagera.
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Kyazi leo Oct 6,2016
Wananchi wa kijiji cha Kyazi, kata ya Kitobo Wilayani Missenyi wakimsikiliza Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala,huu ni mwendelezo program ya Mbunge wa Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa kutembelea Kila Kijiji, Kitongoji na Kata katika Jimbo lake.
Next Post Previous Post
Bukobawadau