Bukobawadau

BALOZI DR KAMALA AFANYA ZIARA YA GHAFLA KATIKA VITUO VYA AFYA-KIZIBA NA MISSENYI !!

Bango la Zahanati ya Kashanga iliyopo katika kata ya Bwanjai.
 Katika kile kinachono amini ni Ufatiliaji wa uwajibikaji katika sekta ya afya Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr Kamala siku ya Jumapili Oct 9,alifanya ziara ya kushtukiza katika Zahanati na Vituo mbalimbali vya Afya vilivyomo katika tarafa za Kiziba na Missenyi.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika Zahanati ya Kashanga iliyopo kata Bwanjai,Pamoja na mambo mengine anabaini zahanati hiyo imekuwa na uhaba mkubwa wa madawa ,Changamoto nyingine kubwa na kubwa na ya muda mrefu zahanati hiyo kwa inaupungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 70.
 Shukuru Stephano pichani ambaye ni Muuguzi/Mkunga wa Zahanati ya Kashanga, Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema zahanati hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa tiba na dawa pamoja na Upungufu wa Watumishi kwa mfano Clinical Officers na mtaalam wa maabara.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge,Balozi Dr. Diodorus Buberwa akimikiliza Muuguzi/Mkunga wa Zahanati ya Kashanga, Shukuru Stephano wakati akitoa maelezo mafupi kuhusu changamoto za huduma ya afya zinazotolewa na zahanati ya Kashanga -Bwanjai
 Shukuru Stephano akijaribu kutoa jibu baada ya kuulizwa walipo wahudumu wengine wa zahanati hiyo.
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa akikagua Kitanda Cha Kujifungulia Akina Mama Wajawazito
 Wa mwisho pichani ni Bwana Changulani akifuatana na Balozi Dr. Diodorus Buberwa na Bi Shukuru  katika kukagua majengo mbalimbali yalioathiriwa na tetemeko la ardhi.
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa akishuhudia namna jiko linalotumiwa na watumishi wa zahanati ya Kashanga lilivyopata nyufa kutokana na tetemeko la ardhi.
Sehemu ya wadau walioambatana na Balozi Dr. Diodorus Buberwa katika ziara hiyo.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa akibadilishana mawazo na Mtawa wa Parokia ya Mugana
 Shughuli inaendelea katika zahanati ya Bugorora
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa anashuhudia Zahanati ya Bugolola ikiwa imefungwa kabisa ''Hamna Dokta wala muuguzi wa zamu''licha ya kuwa ni Jumapili
 Inakuwaje hapa akija mgonja ,wauguzi wakowapi?  Ndivyo anavyosikika Balozi Dr. Diodorus Buberwa akimuuliza mmoja wa majirani karibu na kituo hicho
Mama huyo Jirani pichani kulia anadhibitisha kwamba, Swala la wauguzi wa hapo Bugorora limekuwa la kawaida kwao kuanzia siku za Ijumaa jioni uondoka na kurudi eneo la kazi siku za Jumatatu na hamna hatua yoyote ya kinidhamu inayochukuliwa dhidi yao.
Sasa msafara wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Kamala unaasili katika kituo kikubwa cha Afya cha Bunazi
 Dirisha la Dawa na Sehemu ya kupokelea Wagonjwa Mh. Mbunge anashuhudia hamna lolote wala Chochote, wauguzi hawaonekani kabia
Balozi Dr. Kamala inamladhimu kuelekea kwenye nyumba wanazoishi watumishi wa kituo cha Afya Bunazi na kukutana na mmoja wa wauguzi pichani.
 Kituo cha Afya Bunazi (Misenyi),kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, swala la Maji na huduma duni limekuwa kero kwa wananchi kila anapopita Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Changamoto kubwa kituo hiki cha Bunazi hakina madawa kulingana na mahitaji
 Muonekano wa Majengo ya Kituo cha Afya Bunazi
 Anaitwa M.Said ambaye ndiye Muuguzi wa zamu katika kituo hiki kama anavyo onekana pichani mara baada ya kurejea na kutoa madai kwa Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala kwamba alitoka kidogo kwenda kupata chai.





Next Post Previous Post
Bukobawadau