MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUKOBA VIJIJINI ATEMBELEA KATA ZA RUHUNGA NA KYAMURAILE KUFATIA JANGA KUBWA LA NJAA.
IKIWA ni siku mbili baada ya serikali kuanza tathimini ya jinsi ya
kusaidia kaya za watu 300 wasiojiweza,wakiwemo Wazee,Wagonjwa,Wajane ,watoto
yatima wanaoishi katika mazingira magumu na Walemavu waliokumbwa na tetemeko la
ardhi katika mkoa wa Kagera kata ya Kishogo wilaya ya Bukoba vijijini
imebainika kuandikisha majina hewa ya nyumba saba kwa lengo la Viongozi wa Serikali
za vitongoji na vijiji wajipatie vifaa vya ujenzi kwa njia za udanganyifu.
Udanganyifu huo umebainika katika ziara ya mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini Murshid ngeze alipotembelea kata ya
kishogo kwa lengo la kuelimisha jamii itambue umhimu wa kubainisha kaya za watu
wasiojiweza watakaosaidiwa vifaa vya ujenzi huku akikagua ujenzi wa madarasa
mawili ya muda ili kuwapunguzia adha ya kunyeshewa na mvua wanafunzi baada ya
majengo kubomoka wakati wa tetemeko la ardhi.
Mwenyekiti wa
halmashauri ya Bukoba Vijijini, Murshid Ngeze akiwahutubia waathirika wa Janga la njaa katika kata ya Kyamuraile.
Hata hivyo hayo
yamebainishwa na diwani wa kata kishogo Deogratias Kaijage na baadhi ya
wananchi walisema kuwa orodha ya nyumba zilizoaguka ni nane ila baada ya
kuzitembelea amebaini kuwepo kwa taarifa za uongo ambapo Mwandishi wa mtanzania
ameshuhudia nyumba moja ya mjane ambaye ameshindwa kuijenga kutokana na
umasikini ambae ni Swaumu Isumail maama mwenye watoto watano na wajukuu watatu kwa
sasa wanaishi jikoni.
Haya ndiyo maji yanatumiwa kwa mahitaji mbalimbali kwa Wananchi wa Bukoba Vijijini
Akitoa elimu kwa wananchi mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya bukoba vijijini Murshid Ngeze Alisema
kuwa serikali iliyopo madarakani
imelenga kumsaidia mnyonge huku mwalimu wa shule ya msingi nyamjunanwa Junias
Kashasha aliishukuru kamati ya maafa mkoa wa kagera kwa kujenga majengo ya muda
yatakayosaidia wanafunzi kuepuka jua na mvua wakati wa masomo .
“Pasipokudanganyana wananchi wa Kishogo lengo kuu la
serikali ya awamu ya tano ni kuwasaidia wahitaji walioathika katika tetemeko la
ardhi ndugu zangu tusidanganyane yeyote mwenye uwezo wa kujiongeza katika ujezi
kwa pale alipo athilika katika maafa yaliyotukuta ajitahidi ili kupunguza mzigo
kwa kamati ya maafa”alisema Ngeze
Theonest Rwetabura mkazi wa kata ya Kishogo alisema kuwa
katika zoezi la uhakiki linaloenderea katika jamii yetu ya kuwatafuta wananchi
wanaostahili kusaidiwa vifaa vya ujenzi wanatakiwa kuwa wakweli kwa watathimini
haina maana kudanganya.
“Niiombe jamii na viongozi wa serilikali za vijiji na kata
ili kuwasaidia wenye shida kweli wasio na shida na wamewekwa kwenye utalatibu
watajwe hadhalani ili kuondoa dhana ya kuwanyima haki wahitaji wanaostahili”
alisema Rwetabura.
Pia alisema kuwa Serikali iwafikilie wale wasiojiweza kwa
kaya zenye umasikini uliopitiliza ili kusaidia watu wanaoishi katika mazingila
hatalishi maana kuna familia zingine zinakuwa na watoto wenye uwezo na wengine hazingine hazina wasaidizi kabisa.
Mwisho.