RAIS MAGUFULI AMKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MJANE MKOANI KAGERA.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum
Kijuu akimkabidhi Vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani
Kagera kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli
Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu nyumba aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September.
Nyumba ya Mjane Mjane Agripina Angelo aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September

RAIS MAGUFULI AMKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MJANE MKOANI
KAGERA.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa
vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
Akimkabidi
vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum
Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia
vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya
kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo
mapema mwezi septemba.
Aidha
Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za
kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa
nyumba zao.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa
mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba
yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi
yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.
Vifaa
alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji
mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.