RC ARUSHA NUSRA WAZICHAPE NA MBUNGE LEMA KATIKA UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO
Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,wa kiwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambeye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na mtoto duniani Edru Broun
wananchi waliouthuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
VURUGU kubwa
zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo
la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika
hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la
Arusha.
Vurugu hiyo
zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba
iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo
ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa
imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo
akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge
Lema.
Kabla ya
vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya
Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo
liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la
uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia
afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).
Baada ya
kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe
upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa
hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo
simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na
kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo
la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli
eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya
mda mrefu .
“mkuu wa
mkoa acha kupotosha uma ,mchungaji simamisha hutuba ya mkuu wa mkoa imejaa
siasa anaongea uongo anaongea vitu asivyo vijua,sitakubali huu uongo uendee
siwezi kubali hutuba iendelee kwani anaongea uongo ,akitaka atumie nguvu ya
polisi siogopi kufa ila nataka ukweli ,na aondoe siasa aseme ukweli hili
jamboni lamaendeleo ya wananchi na nikwaifada ya wananchi haswa mama na mtoto
tena wale wasio jiweza kwaiyo naomba mkuu wa mkoa acha uwongo”alisikika Lema
akisema kwa sauti kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa.
Jambo hilo
liliwalazimu baadhi ya wageni wa alikwa wakiwemo wakinamama kumpigia magoti
mbunge huyo alionekana akiwa na jazba kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa
swala ambalo lingeweza kusabisha uvunjifu wa
amani .
Licha ya
Vurugu hizo na kelele za wananchi walionekana nao kupinga hotuba hiyo ya mkuu
wa mkoa,Mkuu wa mkoa wa Arusha aliendelea kuhutubia akiwa anaeleza kuwa eneo hilo lilitolewa na
marehemu Nyaga Mawala kwa serekali ili liendelezwe kwa kujengwa hospitali na mama na mtoto
kitendo ambacho kiliendeleza kelele za wananchi zikipinga hotuba hiyo wakidai
mkuu wa mkoa anapotosha .
“hili jambo
sio la siasa tusiingize siasa ,na kama kunamtu anampango wa kufanya siasa apa
anapoteza muda wake mimi ni mkoa na ninafahamu historia ya eneo hili”alisema
Gambo
Kwa upande
wake mfadhili wa maradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya Festula
Duniani Dkt.Edru Broun alieza
kusikitishwa na tukio lilijitokeza na kuwataka viongozi waweke pembeni siasa
zao na tofauti zao na wamatangulize mungu ili kutimiza shabaha ya ujenzi
wakituo hicho cha hospitali kitakachoweza kumsaidi mama na mtoto.
Alisema kuwa
ujenzi wa hopitali hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni sita na kwa awamu ya kwanza kiasi cha shili
bilioni tatu kitatumika kujenga hospitali hiyo fedha ambazo zitatolewa na
wafadhili kutoka shirika la mama na mtoto (martenity Afrika).
Kwa upande
wake mwenyekit wa Tasisi ya maendeleo ya jiji la Arusha (ARDF) Elifuraha Mtowe
Alisema kuwa eneo la kujegwa hospitali hiyo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala
nakwa ARDF kupitia ofisi ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini ndipo taasisi yao ya ARDF ikamamua kutafuta
mfadhili ndipo walipompata MartenityAfrika.
Alisema kuwa
tangu wampate mfadhili waliingia mkataba na wakakubaliana hospitali iishe ndani
ya mika mitano lakaini mfadhili mwenyewe aliwaakikishia kuwa hospitali hiyo
itaisha mapema iwezeka kwani itakamilika ndani ya mwaka mmoja tu ili mama na
mtoto aweze kupata huduma kwa araka zaidi.
Awali mbunge
Lema aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa mkoa huyo alikuwa amegoma kuja
kuzindua hospitali hiyo hadi pale mbunge huyo alipoamua kumpiga simu katibu
mkuu kiongozi John Kijazi na kumwambia kuwa mkuu wamkoa kagoma kuja
kuzindua hospitali hiyo ndipo katibu
mkuu alipoamua kupiga simu wizara ya tamisema ambapo ndio walimpigia simu mkuu
wamkoa ili aweze kufika kwenye uzinduzi huo.