SERIKALI YAKABIDHI HATI ZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NYAKATO
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua
akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor
, hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato, kutokana na hiyo
na makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga
shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera,
Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam,
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam,
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam,
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI YAKABIDHI HATI ZA UJENZI WA SHULE
YA SEKONDARI NYAKATO
Serikali
imeyakabidhi makampuni ya mafuta ya OILCOM, GBP na MOIL hati za Ujenzi wa Shule
ya Sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera
lilitokea mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano wa hati hizo jijini Dar es Salaam leo Tarehe 23 Oktoba,
2016, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dkt. Hamisi
Mwinyimvua ameyashukuru makampuni hayo kwa ahadi ya kujenga shule mbili
zilizobomoka kutokana na tetemeko hilo.
“Shule
ya sekondari ya Ihungo na Shule ya Sekondari ya Nyakato zilibomoka kutokana na
tetemeko hilo, Kwa kuwa serikali imeanza kujenga shule ya sekondari ya Ihungo
ninawakabidhi nyaraka za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato na ninaamini
mtakamilisha ujenzi kwa wakati ili wanafunzi waweze kurejea shuleni hapo”amesema
Mwinyimvua
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor amesema makampuni yao
yataendelea kuziunga mkono juhudi za serikali za kukabili na kurejesha hali
pindi maafa yanapotokea nchini.
“Sisi
tunaamini nchi yetu ya Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe na sisi
hatunabudi kuwasaidia ndugu zetu wa Kagera kwa athari walizozipata za tetemeko
kwa kujenga shule hiyo kwa ramani ambayo mmetukabidhi” amesema
Mansoor
Naye, Katibu
Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Maimuna Tarish amesema
kuwa jukumu la wizara hiyo ni kutoa elimu bora na ili elimu iwe bora ni lazima
iwepo miundo mbinu ya majengo ya shule ambayo ni bora kama itakayojengwa na
makampuni hayo ya mafuta.
“Tutawakabidhi
michoro ya shule hiyo ambayo ujenzi wake umezingatia ushauri wa wataalamu
wakiwemo wa Jiolojia, aidha katika ujenzi
mtakao kuwa mnaufanya Wakala wa majengo ya serikali (TBA), itasimsmia
kazi ya ujenzi ili kuhakikisha ubora unaotakuiwa unafikiwa” amesema Tarish
Itakumbukwa
kuwa nchi yetu ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika Kanda ya Ziwa na Hasa Mkoa
wa Kagera , Mwezi Septemba mwaka huu. Tetemeko hilo lilikuwa na athari kubwa
kwa miundombinu na majengo ya taasisi mbalimbali za serikali na makazi ya
wananchi.
(Mwisho)