TAARIFA NA RATIBA YA MAZISHI YA OMLANGIRA GOSBART IJUMBA.
Omlangira Rugaibula wa Kanyigo -Missenyi anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Gozbert Ijumba kilichotokea Juzi OCt 4,2016 katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar,Habari ziwafikie ndugu, Jamaa na marafiki popote pale walipo.
Mwili wa Marehemu utawasili mjini kesho Ijumaa Oct 7 na kupelekwa nyumbani kwake 'Nyamkazi' kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho na kufuatiwa na safari kuelekea Kijijini.
Mazishi yamepangwa kufanyika Jumamosi tarehe 8 saa 9 alasili Kijijini Kanyigo-Nyangoma.
#BUKOBAWADAU TUNAMUOMBA MUNGU AIPOKEE ROHO YAKE NA AIPUMZISHE KWA AMANI!!!