WANAWAKE WA KYAMURAILE NA RUHUNGA WAHOFIA NDOA ZAO KUVUNJIKA KUTOKANA NA BAA LA NJAA .
Na mwandishi wetu Bukoba.
WANAWAKE
katika kata ya Kyamuraile na Luhunga Bukoba vijijini mkoani Kagera
wamemulilia mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini Murshid Ngeze
kutokana na Ndoa zao kuwa katika hatali ya kuvunjika kutokana na baa la
njaa kali inayo wakabili.
Kauli
hizo zimetolewa na wanawake hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kata ya Kyamuraile mwenyekiti huyo alipokuwa katika ziara yake ya
kutathimini baa la njaa .
Hata
hivyo wanawake hao ni pamoja na Agnes Balile Jeralidida Joanseni
venansia Domisiani pamoja na sesilia sebasitiani wote wakazi wa kijiji
cha Omkalama kata Kyamulaire.
Agnes
Balile alisema kuwa kutokana na hali ya njaa inayo wakabili wanaume wa
familia wameanzisha tabia ya kuondoka wakidai wanakwenda kutafuta
chakula na kutokomea bila ya kurudi hali inayosababisha wanawake
kulemewa na familia kutokana na ukosefu wa chakula uliosababishwa na
ukame.
Balile
alisema kuwa kutokana na ukame uliopo kwasasa hali ya mashamba
yaliyokuwa yameandaliwa na kupandwa mazao mbalimbali ikiwa ni Mihogo,
Mahindi,Maharage, na Migomba imekauka kiasi kwamba watu wamefikia wakati
wa kula mlo mmoja kwa siku na hata wakati mwingine watu wanalala njaa
hata siku mbili.
"Nikuombe
mwenyekiti wetu wa halimashauri Ngeze fikisha vilio vyetu kwa serikali
watu tuna kufa njaa hatujui hatima yetu na watoto wetu fikilia mimi nina
watoto watano na wajukuu zangu watatu nahangaika jamani hata unga wa
uji unakosa tusaidieni jamani waume zetu wametukimbia na watoto wetu
watanza kutukimbia"alisema Balile
Jeralidida
Joanseni alisema kuwa kutokana na hali ya ukame uliopo wanawake
wanakumbwa na changamoto mbalimbali ambapo inafikia mama anaamua
kuanzisha mahusiano na mwanaume yeyote ili aweze kupata chakula kutokana
na mashamba yao kukauka kwa na ukame kabisa.
Joanseni
alisema kuwa njaa ina sababisha mambo mengi sana ambayo athali zake
zinaweza kutokea kwasasa au badae ambopo yanaweza kulipuka magonjwa na
kuongeza wahalifu kataka jamii kutokana na baa la njaa.
"Nina
amini kuwa hakuna alielileta baa la njaa na sio serikali au mtu yeyote
bali ni mitihani ya mungu hivyo Serikali kuanzia ngazi ya kijiji
wanatakiwa kusaidia maana hali inazidi kuwa ngumu siku hadi siku
kutokana na njaa kali inayo tukabili"alisema Joanseni
Naye
mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini Murshid Ngeze aliwaereza
wananchi hao kuwa swala la njaa lisichanganywe na siasa huu ni wakati wa
kutulia na kujituma katika kazi na kuuomba pasipo kukoma.
Ngeze
alisema kuwa katika baa hili la njaa viongozi wa vijiji na wa kata
wasiutumie matatizo ya wananchi kuwa miladi yao ya kujinufaisha katika
maisha yao na atakae gundulika anafanya hivyo atawajibishwa kisheria.
"Niwatake
akina mama kutulia katika familia zenu na kuiona hii kama changamoto
ambayo ni yamuda mfupi tu na inapita, na mimi ninakwenda kufikisha
tarifa hizi kwa kamati ya maafa ili tuone jinsi ya kusaidia katika hali
hii"alisema Ngeze
Pia
wananchi niwaombe kujenga tabia ya kutunza vyakula vya akiba katika
familia zetu ili inapotokea hali kama hii ya ukame na njaa vyakula hivyo
viweze kutusaidia.
MWISHO.