WATAALAMU WA MAJENGO WA DIT KUFANYA UTAFITI UHARIBIFU WA MAJENGO KAGERA.
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea na Wataalamu wa majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), (hawapo pichani) ambao wapo mkoani Kagera kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili kujua hali halisiilivyo hadi sasa.
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea na Wataalamu wa majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakiongozwa na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa (wa kwanza kulia) ambao wapo mkoani Kagera kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili kujua hali halisiilivyo hadi sasa. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nesphory Bwana akifuatiwa na Dkt. Asinta Manyele na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa wa DIT.
.
(Picha na Eleuteri
Mangi, MAELEZO, Bukoba)
WATAALAMU WA MAJENGO
WA DIT KUFANYA UTAFITI UHARIBIFU WA MAJENGO KAGERA.
Na Eleuteri Mangi,
MAELEZO, Bukoba
Timu ya wataalamu wa
majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wamewasili mkoani Kagera
kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili
kujua hali halisiilivyo hadi sasa.
Timu hiyo
iliyyongozwa na Dkt. Asinta Manyele na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa wa DIT wapo
mkoani humo ili kuwajionea hali halisi ya majengo katika wailaya zilizoathiriwa
na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu na hali ilivyo hadi sasa
baada ya tukio hilo.
Wakiwa katika kituo
cha kukabiliana na maafa mjini Bukoba, wataalamu hao wamemwabia Mkurugenzi
Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kuwa
utafiti wao unalenga kufanya tathmini ya kujua namna nyumba zinavyopaswa
kujengwa ili kukabiliana na atahri za tetemeko la ardhi ambalo kwa Tanzania ni
tukio la kwanza ambalo limekuwa na madhara mengi yakiwemo majengo ya taasisi za
umma na za watu binafsi, nyumba za watu binafsi, miundombinu ya maji, umeme
pamoja na barabara.
Zaidi ya hayo,
watafiti hao wamemwambia Brigedia Jenerali Msuya kuwa nia yao pia ni kuchunguza
aina za udongo katika mkoa wa Kagera na kutoa ushauri wa aina za majengo
yanayotakiwa kujengwa kwa kuzingatia tahadhari za athari za tetemeko la ardhi.
Aidha, watafiti hao
wametoa ushauri kwa waandaaji wa sera, waandae sera inayohusu maelekezo ya
ujenzi wa majengo ambayo yolenga kuhimili athari za tetemeko la ardhi ili
yaweze kustahimili nguvu ya tetemeko la ardhi endapo litatokea.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amewataka
wataalamu hao watumie elimu waliyonayo kuelimisha jamii katika kujua aina ya
majengo wanapojenga nyumba zao ili ziwe imara.
Katika kurejesha hali
baada ya tetemeko hilo, Brigedia Jenerali Msuya amesema kuwa kituo chake
kinashirikiana na Kamati ya Maafa ya Mkoa kwa kuwa na mikutano kila siku pamoja
na kuratibu mambo mbalimbali ikiwemo kupokea na kugawa misaada inayotolewa na
wananchi, taasisi za kidini na za watu binafsi na mataifa mengine yakiwemo
Kenya, Burundi, Uganda, India na Uingereza.
Halmashauri za mkoa
wa Kagera ambazo zimeathiriwa na zaidi na tetemeko la ardhi ni Bukoba Vijijini,
Manispaa ya Bukoba, Muleba, Kyerwa, Misenyi na Karagwe.