WATENDAJI NA VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KUWA WAAMINIFU KATIKA SUALA LA TETEMEKO
WATENDAJI na viongozi wa vijiji wametakiwa kuwa waaminifu katika suala la utambuzi wa
waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera katika kugawa misaada
ya vifaa vya ujenzi ambayo vimenza kutolewa na taasisi binafsi kwa wahanga hao.
Wakizungumza na kwa nyakati tofautiofauti na mwandishi wa gazeti hili
wananchi wa kijiji Mishenyi kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba wathirika hao
walisema kuwa misaada hiyo iliyotolewa hivi karibuni ilitolewa kwa upendeleo na
wengi waliopewa hawakuwa waathirika wa janga la tetemeko na walioathirika
kuachwa.
Kati ya waanchi hao Josephati Rwegoshora mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa
ilitolewa mifuko mitano mitano ya simenti kwa waathirika wa kata hiyo ya
Buterankuzi kwa kaya zipatazo 60 msaada uliotolewa na shirika la World Vision
Tanzania lakini waliopewa sio wote waathirika.
Aliongeza kuwa kulikuwa na kujuana katika kubaini wathirika kwani viongozi wa
kata walibagua baadhi ya watu na kuweka wengine ambao nyumba zao hata nyufa
hazina na kusababisha waliopata madhara kuendelea kuilalamikia serikali.
“Hii misaada ikiwa inatolewa serikali ihakikishe inasimamia kikamilifu hili
zoezi humu kuna suala la watu kujuana na undugu wakati sisi ambao nyumba
zilianguka hatukuwekwa hatujui ni sababu gani imechukulia tuachwe na hawa
watendaji wa kata yetu”alisema Mwananchi
huyo.
Akizungumzia malalamiko hayo Mwenyekiti wa halmashaui ya wilaya Bukoba
Murshidi Ngeze alisema kuwa malalamiko hayo yapo na wamekwisha yafahamu na
wamejipanga kuhakikisha kuwa misaada yote itayotolewa watahakikisha inasimamiwa
kikamilifu ili kuondoa malalamiko hayo.
MWISHO