Bukobawadau

ZIARA YA BALOZI DR KAMALA MINZIRO KIGAZI MISSENYI MAISHA BAADA TETEMEKO LA ARDHI

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameendelea na ziara yake ya kutoapole kwa wananchi kufuatia tetemeko la ardhi mkoani Kagera lililotekea mwezi mmoja uliopita, tareh 10 Sep,2016. Balozi Dr. Kamala mara baada ya kuzungukia taasisi mbalimbali na Nyumba za makazi kujionea athari pia umefanyika mkutano wa hadhara, uliofanyika shule ya Msingi Kiwelu Minzoro Wilayani Missenyi.
Wananchi wa Vijiji hivyo na Viongozi wao wakiongea na Balozi Dr.Kamala wanabainisha changamoto wanazopambana nazo baada ya kutokea kwa Tetemeko la ardhi,inaonekana ni kama taarifa za maafa haziendi Sawasawa

 Muonekano wa tent walilojengewa wananchi hawa kutoka kwa ndugu zao wanaoishi nchi jirani ya Uganda.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiongozana na  Mh. Twaha Diwani wa Kata Minziro
  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala hii ikiwa ni ziara yake ya pili tangu kutokea kwa #Tetemeko la ardhi akiakisha amepata tathmini ya kweli ili kupata nini cha kuhoji Bungeni.

Pichani kushoto ni Deocles Modest Mtendaji wa Kijiji Kigazi -Minziro

 Bi Paulina John pichani kushoto na mme wake Mzee John Bagandaswa wakati wakielezea changamoto walizonazo mara baada ya kuanguka kwa nyumba yao kuanguka na sasa wanajiegesha kwenye banda la muda
 Katika picha ya pamoja Mbunge wa Jimbo la Nkenge Dr. Diodorus Buberwa Kamala(katikati) na familia ya Mzee Mzee John Bagandaswa ambaye ni balozi wa Shina  kitongoji Bilongo Kijiji Kigazi kata ya Minziro
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kutoa pole kwa wakazi wa Kijiji cha Bilongo-Minziro
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kutembelea Kaya mbalimbali kujionea athari ya Tetemeko la Ardhi.
 Picha inaongea kwa hali ya kawaida lazima Mbunge awe upande wa Wananchi waajili wake,ndivyo anavyo onekanana Mh.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala katika hali ya mshangao..!!

 Wanamama wakazi wa Kijiji Minziro kama walivyokutwa na Camera yetu
Muonekano wa Makazi ya wananchi yakiwa yamearibika kufuatia Tetemeko la Ardhi
 Kwa upande mwingine shughuli za kilimo zikindelea
 Watoto wakiwa katika utaratibu wao kawaida masikani
 Wataalam wa Jiolojia wanasema katika Kijiji hiki cha Kigazi Kata ya Minziro Wilayani Missenyi ndipo lililipo anzia tetemeko la ardhi.
 Kwa ufupi ni kwamba athari ni kubwa tena sana
 Bi Jasinta Vicent (55) ambaye ni Mjane akiwa anamuonyesha Mbunge wake Picha za Mawaziri walioweza kuwatembelea na kuwapo pole kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Sep 10,2016.
Hivi ndivyo Nyumba ya Mjane Jasinta Vicent (55) ilivyobomoka
 Mtaa kwa mtaa Nyumba kwa Nyumba katika kutoa mkono wa pole kwa wananchi wa Minziro Wilayani Missenyi ndivyo anavyo onekana pichani Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Mbunge wa Nkenge akiendelea kutoa mkono wa pole kwa waathirika wa tetemeko
Eneo la mpakani Minziro,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akibadilishana mawazo na Polisi wa Uganda
Hapa panaitwa Kijiji Kigazi Kata ya Minziro Wilayani Missenyi Kwenye gogo lililolala ndiyo alama iliyowekwa na Wataalam wa Jiolojia Kuwa Tetemeko lililotokea tarehe 10.09.2016 mkoani Kagera lilianzia hapa na Wataalam hao wanasema miamba iliyosuguana ipo kilometa 36 kutoka usawa wa ardhi.
 Bi Beath Lameck muuguzi wa kituo cha Afya minziro akimuonesha maeneo yenye nyufa Mh. Balozi Dr. Kamala.
 Jengo la Zahanati ya Kata Minziro ambayo baadhi ya sehemu zimeathiriwa tukio la Tetemeko la ardhi
 Wanamama kama walivyokutwa Katika Zahanati ya minziro
 Mbunge wa Nkenge akiwajulia hali baadhi ya Wagonjwa aliowakuta katika Zahanati ya Minziro alipofika akiwa katika ziara yake ya kutoa pole kwa waathirika wa Tetemeko la ardhi
 Bi Beath Lameck muuguzi wa kituo cha Afya minziro
 Balozi Dr. Kamala akikagua maeneo mbalimbali ya Zahanati yaliathirika na Tetemeko la ardhi.
 Taarifa ya Kata ya maendeleo ya Kata Minziro
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Shule ya Msingi Kiwelu
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kufatilia mkutano huo
 Muendelezo wa matukio ya picha katika mkutano wa balozi Dr. Kamala na wananchi wa Kijiji cha Rugazi
Balozi Dr. Kamala anandelea na ziara yake kwa kutembelea Kata zote na Vijiji ndani ya Jimbo la Nkenge..
 Wananchi mara baada ya mkutano na kutoa hoja kwa mbunge wao
#Bukobawadau#TetemekoKagera
Next Post Previous Post
Bukobawadau