BARABARA YA KIBETA YASEMEKANA KUKITHIRI KWA AJALI
Ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo zinatokana na uzembe unaofanywa na madereva au watembea kwa miguu kwa kutozingatia ,hivyo Wananchi wa Kibeta wanaomba Mamlaka usiku kuchunguza kiini cha ajali hizo na kuomba kuongezewa matuta kati ya eneo la kwa Mbunge wa Jimbo lao na njia panda ya kuelekea Rugabwa kutokana na kukithiri kwa ajali katika eneo hilo katika vipindi tofauti.
Ajali za barabarani zimekuwa ni janga kubwa kwa taifa letu. Ajali hizi kwa muda wa hivi karibuni zimeongezeka sana na kusababisha watu kufariki dunia, kupotelewa mali, kupata majeraha, kupata ulemavu wa kudumu na watu wengi wamejikuta maskini kwa sababu ya ajali za barabarani.
Tofauti na barabara hii ya kibeta,kumekuwepo na wimbi la ajali za mara kwa mara katika eneo la Rwamishenye kwa Kagambo na eneo Rwamishenye (round about) ukizingatia Ajali za barabarani zina madhara makubwa kiuchumi na Mkoa wetu upo hoi