MKOA WA KAGERA TARATIBU WAANZA KUREJEA KATIKA ENZI ZA NSHOMILE KATIKA ELIMU WASHIKA NAFASI YA TANO KATIKA KUMI BORA KITAIFA DARASA LA VII
Na:
Sylvester Raphael
Kutokana na usimamizi na uongozi
thabiti chini ya Mkuu wa Mkoa mahili wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kiwango
cha Elimu mkoani hapa kimeanza kupanda
kwa kasi na kuifanya Kagera kuanza kurejerea katika miaka ya 1980 wakati ule
mkoa ulipokuwa unasifikakwa jina la “Nshomile”
Katika matokeo ya darasa la saba
ya mwaka 2016 Mkoa wa Kagera umeendelea kufanya vizuri na kushika nafasi ya tano kati ya mikoa 10 bora,
Aidha mwaka 2014 Kagera ilishika nafasi ya 10 kati ya mikoa kumi bora, mwaka 2015 mkoa ulishika nfasi ya 7 kati ya
mikoa 10 bora na mwaka huu umepanda juu nafasi mbili za ufaulu.
Halmashauri iliyoongoza katika
mkoa wa Kagera ni Ngara iliyofaulisha kwa asilimia 87.82% na kitaifa imekuwa ya
12, mwaka jana 2015 ilikuwa ya 18. Ya pili ni Biharamulo iliyofaulisha kwa
asilimia 85.11% na kitaifa imeshika
nafasi ya 21, mwaka jana ilikuwa ya 3. Halmashauri ya tatu kimkoa ni Muleba
liyofaulisha kwa asilimia 83.69% na kitafa kushika nafasi ya 24 ambapo mwaka
jana 2015 ilishika nafasi ya 43.
Halmashauri ya nne ni Manispaa ya
Bukoba iliyofaulisha kwa asilimia 83.23% na kushika nafasi ya 26 kitaifa aidha,
mwaka jana ilishika nfasi ya 47. Ya tano ni Missenyi liyofaulisha kwa asilimia
78.80% na kushika nafasi ya 46, mwaka jana ilikuwa ya 19. Kyerwa ya sita
imefaulisha kwa asilimia 77.60% na kushika nafasi ya 53 ambapo mwaka jana 2015
ilishika nafasi ya 68 kitaifa.
Karagwe ya saba iliyofaulisha kwa
asilimia 76.79% na kushika nafasi ya 54 kitaifa ambapo mwaka jana 2015 ilishika
nafasi ya 72 kitaifa. Halmashauri ya mwisho ni Bukoba iliyofaurisha kwa
asilimia 74.86% na kushika nafasi ya 69 kitaifa ambapo mwaka jana ilishika
nafasi ya 102, aidha, imepanda nafasi 33 kitaifa japo imekuwa ya mwisho katika
mkoa wa Kagera. Shuleiliyoongoza mkoani Kagera na kuwa katika shule 10 bora zilizofanya
vizuri kitaifa ni St. Achileus Chiwanuka
kutoka Wilaya Muleba .
Akiongelea matokeo hayo Afisa
Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Aloyce Kamamba alisema mkoa wa Kagera unaendelea
kufanya vizuri na miaka ijayo mkoa huu utaweza kushika nafasi ya kwanza kama
ilivyokuwa zamani. Aidha, Afisa Elimu kamamba alisema yeye na wataalam wake watafanya
tathmini ya kina kujua kwanini Halmashauri ya Biharamulo imeshuka katika ufaulu
ukilinganisha na mwaka jana .
Bw. Kamamba aliipongeza
Halmashauri ya Bukoba kuwa pamoja na kushika nafasi ya mwisho katika mkoa kama
mwaka jana lakini imepandisha asilimia za ufaulu aidha, imepanda nafasi 33
kitaifa. Bw. Kamamba alisema kuwa juhudi za walimu zimeonekana lakini akatoa
wito kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha inaongeza juhudi ili iweze kutoka nafasi
ya mwisho kimkoa.
Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Mwl. Aloyce Kamamba.
Katika hatua nyingine Afisa Elimu
Bw. Kamamba alisema mkakati wa mkoa ni kuhakikisha Kagera inashika nafasi ya
kwanza kitaifa ambapo yeye pamoja na timu yake ya Elimu chini ya uongozi wa
mkuu wa Mkoa wa Kagera wataendelea kufanya usimamizi wa kina ili kuhakikisha
kiwango cha elimu kinaendelea kupanda mkoani Kagera.
Mikoa kumi iliyofanya vizuri
kitaifa ni Geita iliyofaulisha kwa asilimia 86.92% mwaka jana 2015 ulishika
nafasi ya 6. Wa pili ni katavi uliofaulisha kwa asilimia 86.80%, mwaka jana
ulikuwa 1, Iringa ulishika nafasi ya 3 na ulifaulisha kwa asilimia 82.87%,
mwaka jana ulikuwa wa 10. Dar es Salaam umeshika nafasi ya 4 kwa kufaulisha kwa
asilimia 82.59%, mwaka jana ulishika nafasi ya 2. Kagera numeshika nafasi ya 5
kwa kufaulisha kwa asilimia 80.99% na mwaka jana ulishika nafasi ya 7.
Mkoa wa sita ni Mwanza
uliofaulisha kwa asilimia 79.13%, mwaka jana ulikuwa wa 3 kitaifa. Kilimanjaro umeshika nafasi ya 7 na kufaurisha
kwa asilimia 79.10%, mwaka jana ulikuwa wa 4. Arusha umekuwa wa 8 kwa kufaurisha
kwa asilimia 77.58%, mwaka jana ulishika nafsi ya 5. Njombe umekuwa wa 9 kwa
ufaulu wa asilimia 77.10% na mwaka jana ulikwa wa 9. Tabora umekuwa wa 10 kwa
ufaulu wa asilimia 71.35% na kushika
nafasi ya 10aidha mwaka jana ulikuwa
mkoa wa 25, wa pili kutoka mwisho.