MZAZI ANAYEPELEKA MTOTO WAKE SHULE BUBU ZISIZOSAJILIWA KUCHUKULIWA HATUA PAMOJA NA MWENYE SHULE
Na MatukiodaimaBlog
KUFUATIWA uwepo wa
utitiri wa shule binafsi za awali na msingi za English Midium au
kiswahili Midium School maeneo mbali mbali mkoani Iringa wazazi
mkoani hapa waonywa kuacha kuwaandikisha watoto wao katika shule
hizo bubu zisizosajiliwa ili kuepuka kuchukuliwa hatua mzazi na
mmiliki wa shule husika.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake jana naibu mthibiti
mkuu ubora wa shule kanda ya nyanda za juu kusini Aldo Masonda
alisema kuwa mzazi kabla ya kumpeleka mtoto wake kuanza elimu
ya awali ama ya msingi kwenye shule yoyote ni lazima kuomba
kupatiwa namba ya usajili wa shule husika kabla ya kumwandikisha
mtoto na iwapo atakuwa na hofu na namba ya usajili wa shule husika
afike ofisi za mratibu elimu kata ama ofisi za elimu wilaya na mkoa
kuweza kupata uhakika wa usajili wa shule husika.
Hivyo
alisema ni kosa kwa mzazi kumpeleka mtoto shule isiyo sajiliwa
na kuepuka kuwajibishwa mzazi na mmiliki wa shule hiyo ni vizuri
wazazi kufika ofisi za elimu kujiridhisha ama kufika ofisi ya
mthibiti ubora wa shule ngazi ya wilaya au ofisi ya kanda na kwa
wale wanaoweza kuingia katika tovuti ya wizara ya elimu ambako
wataona shule zote nchi nzima ambazo zimesajiliwa na zina sifa ya
kuitwa shule .
Alisema
kumezuka tabia ya watu kuendesha shule pasipo kuwa na usajili jambo
ambalo ni kosa la kisheria na iwapo itabainika mhusika
atachukuliwa hatua na kuwa tayari katibu mkuu wa wizara amekuwa
akichukua hatua mbali mbali ya kuwaandikia barua wale wote
wanaoendesha vituo vya elimu wanavyoviita ni shule za English Midium
.
Masonda
aliwataka wananchi wote kuendelea kutoa taarifa katika ofisi yake
iwapo watabaini kuwepo kwa shule bubu katika maeneo yao kwani kwa
kimsingi ni marufuku kwa mtu yeyote kutoa elimu kuanzia watoto saba
na kuendelea kwa kuwa iwapo itabainika kuwa mtu anatoa elimu kwa
watoto kuanzia saba na kuendelea bila kuwa na namba ya usajili ni
kosa .
Alitaja
sifa ya kuitwa shule ni pamoja na kuwa na vyumba vya madarasa
vizivyopungua saba ,vyoo matundu yasiyopungua 10 ,ofisi za walimu
tatu pia kuwa na ardhi yenye ukubwa kuanzia heka tatu ila alisema
wapo baadhi ya watu wamekuwa wakivunja sheria kwa kuanzisha
shule bila ya kuzingatia taratibu .
Kuhusu
mambo kumi muhimu ya kuzingatia katika usajili wa shule alisema
ni pamoja na andiko la mradi ,hati miliki ya kiwanja ,kibali cha
kujenga shule ,site plan ya shule ,barua ya uthibitisho wa kuwa
mwenye shule ,barua ya uthibitisho kuwa meneja wa shule ,taarifa
ya mhandisi wa majengo wilaya ,taarifa ya bwana afya wilaya ,taarifa
ya ukaguzi wa mwisho wa shule ,orodha ya majira ya walimu na vyeti
vyao ,mikataba ya ajira ya wafanyakazi na fomu ya usajili wa shule
(form no RS 8)
Hivyo
alisema iwapo kuna shule imeanzishwa na inapokea wanafunzi
pasipo kufuata taratibu hizo kumi katika uanzishwaji wake mmiliki
wa shule hiyo atakuwa amevunja sheria na ikibainika atawajibishwa
kisheria japo aliwataka wananchi kuendelea kuwekeza katika sekta
ya elimu kwa kujenga shule ila kwa kufuata taratibu zote .
Masonda
alisema wao wanasimamia ubora wa shule zote kuanzia shule za
awali hadi vyuo vya ualimu vya binafsi na serikali na kuwa
changamoto kubwa wamekuwa wakiipata kwa taasisi binafsi kwa baadhi
ya watu kuanzisha kuanzisha shule bubu.
Kutokana
na uchunguzi uliofanywa na mtandao wa matukiodaimaBlog katika
mkoa wa Iringa kumekuwepo kwa shule zinazoendeshwa pasipo
kusajiliwa huku wazazi wakitozwa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya
kulipia ada .
Usikose wiki Alhamisi wiki ijayo mwendelezo wa habari hii