TEA NA CRDB YAKABIDHI VITANDA NA MAGODORO SHULE YA SEKONDARY PANGANI
Meneja
Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe
akisaini kitabu cha wageni wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka
24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la
wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani
Pwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi. Rosemary Msasi akongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto kike na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani na kuwataka wanafunzi watakaotumia bweni hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu ili kuwawezesha wengine kulitumia
Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wakike katika shule hiyo ikiwamo kusafiri umbali mrefu kuja shuleni.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa anaamini lengo la mradi huo lenye dhumuni ya kumuendeleza mtoto wa kike litasaidia kuondo chagamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wa kike kwa muda mrefu.
Kaimu
Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiwaonesha Meneja Elimu,
Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe(mwenye
nguo nyeupe) na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi (katikati
mwenye nguo nyeusi) moja ya bweni la wanawake lenye vitanda na magodoro
walivyotoa katika shule ya sekondari pangani mkoani Pwani.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiwashukuru Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe (mwenye nguo nyeupe) na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi (katikati mwenye nguo nyeusi) kwa masaada wa vitanda 24 na magodoro 48 yaliyogharimu milioni 18 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi. Rosemary Msasi akongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto kike na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani na kuwataka wanafunzi watakaotumia bweni hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu ili kuwawezesha wengine kulitumia
Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wakike katika shule hiyo ikiwamo kusafiri umbali mrefu kuja shuleni.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa anaamini lengo la mradi huo lenye dhumuni ya kumuendeleza mtoto wa kike litasaidia kuondo chagamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wa kike kwa muda mrefu.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiwashukuru Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe (mwenye nguo nyeupe) na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi (katikati mwenye nguo nyeusi) kwa masaada wa vitanda 24 na magodoro 48 yaliyogharimu milioni 18 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Meneja
Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe na
Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi,walimu na viongozi wa mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi
Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48
kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo
Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
(PICHA NA KITENGO CHA
HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA)
Na Mwandishi Wetu-TEA
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa
kushirikiana na Benki ya CRDB wamekabidhi Magodoro 48 na Vitanda 24 kwa ajili
ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo mkoani Pwani.
Akiongelea kuhusu mradi huo
uliogharimu shilingi milioni 20 Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary
Nchimbi amesema kuwa lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya
kusaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wakike katika shule
hiyo ikiwamo kusafiri umbali mrefu kuja shuleni.
“Hii ni mwanzo tu sisi kama CRDB
tutaendelea kushirkiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kutekeleza miradi
mingine na lengo letu kubwa ni kusaidiana na serikali katika kuinua kiwango cha
elimu nchini,” Alisema Bi. Rosemary
Kwa upande wake Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa
Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe amewataka wanafunzi watakaotumia
bweni hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu ili kuwawezesha wengine
kulitumia.
Bi. Sylvia alisema kuwa “ Tunafahamu
zipo changamoto nyingi zinazoikabili Sekta ya Elimu nchini, ikiwamo changamoto
ya miundombinu hasa kwa wanawake hivyo Mamlaka ya Elimu itaendelea kufadhili
miradi yenye lengo la kuinua ubora wa elimu ikiwemo mkakati wa kusaidia watoto
wa kike”.
Akizungumzia kuhusu ufadhili huo
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango amesema kuwa anaamini
lengo la mradi huo wenye nia ya kumuendeleza mtoto wa kike utasaidia kuondoa
chagamoto zilizokuwa zikiwakabili wanafunzi hao kwa muda mrefu.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi. Rosemary Msasi amesema kuwa ujenzi wa
miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto
kike na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Diwani wa Kata ya Pangani Bw.
Augustino Mdachi alizishukuru Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa
kushirikiana na Benki ya CRDB kwa kusaidia kuondoa moja ya kilio kilichokuwa
kinaikabili shule hiyo.
Utekelezaji wa Mradi huu ni mwendelezo
wa moja ya mkakati wa kusaidia watoto wa kike unaotekelezwa na Mamlaka ya Elimu
Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.