TFS WAENDELEA KUTOA MBEGU KWA VIKUNDI MBALIMBALI
NA MWANDISHI WETU
Bukoba.
WAKARA
wa huduma za misitu Tanzania (TFS) wanaendelea kutoa mbegu za viriba
kwa vikundi mbalimbali na tasisi pamoja na watu binafisi wenye vigezo
ili waweze kupanda miti na kurudisha misitu ya asiri ambayo imetoweka.
Hata
hivyo Meneja wa (TFS) wilaya Bukoba Braison Paul Mkiwa alisema kuwa ili
mtu awenavigezo vya kupewa mbegu hiyo ya seriklai anatakiwa kuwa na
shamba lakutosha pamoja na utambulisho wa serikali ya kijiji au kata.
Hata
hivyo alisema kuwa mbegu hizo zimetolewa katika maeneo manne mpaka sasa
ambapo ni shule ya sekondali Bukara, E.L.C.T Bukoba, Neema group na kwa
mtu binafsi Adiventina Kamungi.
Aidha
Mkiwa alisema kuwa Serikali kuu kupitia wakala wa huduma za mistu
wamekuwa wakitoa mbegu bure kwa wananchi wanaojishughulisha na kilimo
cha misitu pamoja na viriba.
Mkiwa alisema katika halmashauri ya Bukoba vijijini zimetolewa mbegu kilo nne na viriba kilo 28 .
Pia
alisema kuwa Serikali kwa kujali mahitaji ya wakulima wa misitu ambayo
inazinunua mbegu hizo kwa kilo moja shilingi milioni Moja ambapo jumla
ya mbegu hizo kilo nne ina thamani ya shilingi milioni nne.
Alisema
kuwa viliba vina nunuliwa kwa thamani ya elfu kumi kwa kilo ambayo
imegarimu shilingi laki mbili na themanini ambayo imeshatolewa kwa
maeneo hayo manne.
Mkiwa
alisema kuwa mbengu hizo zimetolewa kilo nne tu ambazo mpaka sasa kwa
thamani yake ni shilingi milioni nne tu ikiwa kwa kilo moja inauzwa kwa
shilingi milioni moja.
"Wananchi
watambue kuwa kilimo hiki cha upandaji miti ni bora sana kuliko watu
wanavyo fikiri, na pia wananchi waje wachukue mbegu kwani mbegu
zinatolewa bure na serikali hakuna hata senti inayolipwa ili mwananchi
apate mbegu"alisema Mkiwa.
Naye
mkulima wa misitu Jonasi Mashaka mkazi wa wilaya ya Bihalamuro Kiruruma
alisema kuwa kilimo cha misitu ni nibora kama yalivyo mazao mengene
hivyo wananchi na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuwekeza katika kiliomo
hicho.
Mashaka
alisema kuwa kilimo cha misitu kinasaidia kuwa na uchumi usio yumba
katika familia kwani miti inapo vunwa pale inapo kuwa imekomaa na
kuzalisha vitu mblimbali kishelia inasaidia kwa kusomeha watoto na hata
kujenga nyumba bora.
"Mimi
binafsi nimekuwa nikipanda miti na baadhi ya watu wakinibedha lakini
nilipo anaza kuvuna na kuwapeleka watoto wangu katika shule za thamani
imekuwa i hudhuni kwa waliokuwa wakiona kuwa napoteza muda tu"alisema
Mashaka.
Mashaka
aliongeza kuwa jamii itambue kuwa kilimo cha misitu ni cha muda murefu
sana lakini pia faida yake ni kubwa mmno tofauti na mazao mengine.
Shirika
hilo limedhamilia kurudisha misitu ya asili ambayo imetoweka kutokana
na uvunaji ovyo unaotokana na watu wanaohujumu maliasili hiyo kila mara.
Mwisho.