WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 WAANZA KAMBI
Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Universe
Tanzania 2016 wakiwa wamesimama mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana,Fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo
Oysterbay.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications
L.T.D,Maria Sarungi Tsehai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana,kuhusu kuanza kambi kwa warembo wa Miss Universe Tanzania
2016 ambapo fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo
Oysterbay. Kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Collessium,Mustafa Dhanji na
Mratibu wa shindano hilo,Mwanakombo Salim.(PICHA NA ELISA SHUNDA)
NA ELISA SHUNDA,DAR
Warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 wameanza rasmi
kambi katika hoteli ya Colessium hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali za
mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 jijini Dar es Salaam katika
Ukumbi wa hoteli hiyo iliyopo Oysterbay.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa
ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake hususani
katika ujasiriamali, urembo na haiba . Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na
wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana,Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na muandaaji
mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa shindano
la mwaka huu litakuwa zuri na la kipekee.
“Shindano la mwaka huu la Miss Universe Tanzania 2016
tumefanya usaili ambao ni mzuri sana lakini pia katika mfumo tofauti ukilinganisha
na ilivyozoeleka warembo wetu wameonyesha vigezo vyote walivyoagizwa watume
ambapo pamoja na kutuma video zao wakijibu maswali waliyotumiwa na kisha kuchujwa
kwa kufuata mfumo huo lakini pia mkumbuke kuwa shindano hili la Miss Universe Tanzania
tangu kuanzishwa kwake limefanikiwa kuifikia mikoa sita ikiwemo Dar es salaam,
Dodoma, Arusha,Mwanza,Iringa na Mbeya” Alisema Sarungi
Kambi ya Miss
Universe Tanzania 2016 imekamilishwa na warembo 10 ambapo waliofanikiwa kupata
uwakilishi ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mbeya.
Aidha mashindano hayo yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo
mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa
Taifa pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa
mwanamitindo wa kimataifa,wengineo waliofanikiwa kuchukua taji la Miss Universe
Tanzania ni Amanda Ole Sulul 2008,Illuminata James 2009,Hellen Dausen
2010,Nelly Kamwelu 2011,Winfrida Dominique 2012,Betty Boniface 2013,Caroline
Benaed 2014 na Lorraine Marriot mwaka 2015 ambaye ndiye atakayekabidhi taji kwa
mshindi wa mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Best
Western Plus Collesium Hotel, Compas Communications, Kwanza Tv na New York Film
Academy.
Mwishoooooo