UJIO WA HUDUMA YA (SPEED BOAT) KATIKA ZIWA VICTORIA!!
Habari
kubwa kutoka katika Chanzo makini ni Ujio wa Boti mpya inayoenda kwa mwendo kasi (Speed boat) hivi karibuni,kama inavyosemekana kumba huduma ya Boti hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ya Usafiri katika Ziwa Victoria,Boti hiyo ya
Kampuni binafsi ya Equetorial Wild Safaris ya nchini Uganda inatalajia
kuanza safari zake kati ya Bukoba na Mwanza.Kama inavyo onekana pichani
ikiwa katika majaribio ya awali.
Pamoja na mambo mengi mengine Boti hiyo itakuwa Kichocheo cha kuongezeka kwa watalii wanao pitia Entebe /Uganda kutembela hifadhi ya Serengeti.
Wakati huo wananchi wa Mkoa wa Kagera wanaendelea kusubilia kwa hamu ahadi ya SERIKALI kuwaletea meli kubwa itakayoweza kukidhi haja ya usafiri wa majini iliopo na tayari Bilioni 21 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya zitakazotumika katika Ziwa Victoria
#Bukobawadau
Credit photo @tanzanaire